Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Zaidi ya shilingi milioni 800 kutumika ujenzi wa kituo cha afya Kisiwa cha Ukara

Imewekwa tar.: November 18th, 2018

Imeelezwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 800 zinategemewa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Bwisa kilichopo  katika Kisiwa  cha Ukara  ikiwa ni ahadi  aliyoitoa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati ilipotokea ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo mapema leo,wakati akizundua  rasmi ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisa kilichopo Kisiwani Ukara.

Ahadi hiyo ya Rais Magufuli ilielekeza pamoja na mambo mengine kutumia sehemu ya fedha za rambirambi takribani milioni 856 kuboresha, kuimarisha na kupanua miundombinu ya kituo cha afya bwisya kifikie hadhi sawa na hospitali ya wilaya kwa lengo la kusogeza huduma bora ya afya kwa wananchi wa kisiwa hicho wapatao 44,000 ambao wapo mbali na hospitali ya wilaya.

Mhe. Jafo alikagua na kuzindua rasmi shughuli za ujenzi wa hospitali hiyo inayojengwa na kusimamiwa na jeshi la wananchi Tanzania chini kikosi cha SUMA JKT.

Akihutubia wananchi wa kisiwa cha Ukara, Mhe Jafo alisisitiza kuwa wajenzi wazingatie ujenzi wa majengo yenye viwango na kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati shughuli hiyo.

"Ni matumaini yangu kuwa ifikapo Mwezi Februari, 2019 kazi hii itakuwa imekamilika kwa kiwango kinachokubalika. Kwa uzoefu wenu katika miradi na operesheni kama hizi Sina shaka SUMA JKT mtafanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa na uzalendo ili kutimiza ahadi na ndoto ya Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli kwa wana ukara na watanzania wote kwa jumla" alisisitiza Jafo

Mhe. Jafo amesema kimeundwa kikosi kazi maalum chenye wataalam kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo jeshi la wananchi wa Tanzania, wataalam wa sekretariati ya Mkoa, Halmashauri za Mkoa wa Mwanza na taasisi zingine za Serikali kitakachosimamia ujenzi huo kwa umakini mkubwa kikiongozwa na Luteni Hamis Masoud.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe mongella alifafanua kuwa imeelekezwa mafundi na vibarua wote watoke miongoni mwa wananchi na wakazi wa kisiwa cha ukara na maeneo jirani ili kuzalisha ajira na ujira kwa wazawa.

Amesema tayari manunuzi ya vifaa vya ujenzi umefanyika ambapo mkoa ulisimamia jambo hilo kwa kuagiza bidhaa moja kwa moja toka viwandani ili kupunguza gharama za ujenzi wa hospitali hiyo, alisema mongella.

Aidha kisiwa cha Ukara ni miongoni mwa visiwa 38 vinavyounda wilaya hiyo ambapo kati ya hivyo, visiwa 25 ni makazi ya kudumu ya watu na visiwa 13 ni makazi yasiyo ya kudumu.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.