Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Ummy azionya halmashauri zilizokusanya chini ya asilimia 75

Imewekwa tar.: April 23rd, 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Halmashauri ambazo   zimekusanya mapato  chini  ya asilimia 75 ya makisio yake kufanya tathmini na kuhakikisha inaweka  mikakati  madhubuti ya kufikia malengo  yao ifikapo  30  Juni,  2021.

Akitoa taarifa  ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri  kwa kipindi cha Julai, 2020  hadi machi, 2021  Waziri ummy  amesema  kila Halmashauri  ihakikishe inatumia kwa usahihi mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato  ya  ndani  na mifumo ya uhasibu  ili kutoa taarifa kwa kufuata matakwa  kwa kuzingatia  viwango vya kimataifa  vya uhasibu katika sekta ya umma (IPSAS).

Waziri Ummy ameiagiza Mikoa kuendelea kusimamia, kutoa ushauri na maelekezo kuhusu suala zima la ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani ya Halmashauri   kabla ya viongozi wa juu kubaini matatizo ya halmashauri nchini.  

Amezielekeza Halmashauri zote nchini kuzuia na  kudhibiti matumizi ya fedha mbichi  kabla ya makusanyo  hayajapelekwa benki, kwa kuwa kwa mujibu wa sheria fedha inatakiwa kukusanywa na kupelekwa benki ndipo kuanza kutumika.

Waziri Ummy amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kutumia fedha mbichi za makusanyo kabla ya kupelekwa benki na atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake kwa kuwa atakuwa amekiunka miongozo ya kifedha inayomtaka kuhakikisha wanankusanya na kupeleka benki ndipo kuanza kutumika.

Ameielekeza Mikoa kuendelea kusimamia Halmashauri  kwa kutoa taarifa kupitia mifumo ya kielektroniki, kusisitiza usuluhishi wa taarifa na usahihishaji wa takwimu  katika  mifumo mbalimbali  na kuongeza jitihada katika usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hata hivyo,  amezitaka Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha wanatoa  ushauri stahiki kwa wakati, kutatua changamoto zilizopo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato katika halmashauri wanazoziongoza, kutoa miongozo  kwa lengo za kuhakikisha Mamlaka za  Serikali za Mitaa zinafanya vizuri katika suala zima la ukusanyaji wa mapato ili kuleta maendeleo kwa wananchi

Akizungumzia ukusanyaji wa Mapato hayo Waziri Ummy ameeleza kwa mwaka wa fedha 2020/21 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 814.96 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 Halmashauri zimeweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 557.45  sawa na asilimia 68 ys  makisio  ya mwaka

Amefafanua kuwa taarifa za mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri katika kipindi cha Julai  2020 hadi Machi, 2021 imeonesha uwepo wa ongezeko la mapato yaliyokusanywa kuwa ni shilingi bilioni 30.14 ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho cha Julai – Machi , 2020 sawa na ongezeko la asilimia 6.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 117 ya makisio yake ya mwaka wakati Halmashauri za Wilaya za Ngorongoro imekuwa ya  mwisho kwa kukusanya chini ya asilimia 34 ya makisio yake ya mwaka.

Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi bilioni 52.78 na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 453.72

Hata hivyo katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo Waziri Ummy  amebainisha kuwa Mkoa wa  Geita umefanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo umekusanya kwa wastani wa asilimia 82 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo wakati Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa  Singida  ambao umekusanya wastani wa asilimia 48 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy  ameweka wazi Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa Kuzingatia Wingi wa Mapato kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kigezo cha wingi wa mapato ambapo imekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 133.90 huku Mkoa wa mwisho katika wingi wa mapato ni Mkoa wa Rukwa ambao umekusanya Shilingi Bilioni 5.57.

Vile vile Ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa Kuzingatia aina ya Halmashauri kwa Kigezo cha asilimia ya makusanyo ukilinganisha na makisio ya mwaka Waziri Ummy amesema kwa upande wa Majiji Halmashauri ya Dar-es-salaam imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 78 ya makisio yake ya mwaka na Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya kwa asilimia 58 ya makisio yake ya mwaka.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa ambayo imekusanya asilimia 101 ya makisio yake na Katika kundi hilo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya kwa asilimia 36 ya makisio yake ya mwaka.

“Kwa kundi la Halmashauri za Miji , Halmashauri ya Mji Kibaha  imeongoza kwa kukusanya kwa asilimia 93 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Halmashauri ya Mji wa Bariadi imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 36 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2020/21” amesema Waziri Ummy

Aidha, kwa upande wa Halmashauri za Wilaya amesema Halmashauri ya Wilaya ya  Msalala imeongoza kwa kukusanya asilimia 117 ya makisio ya mapato ya ndani huku Halmashauri za Wilaya za Ngorongoro kuwa ya mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya  asilimia 34 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa Fedha 2020/21.

“Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam a imeongoza kwa kundi la Halmashauri za Majiji kwa kigezo cha wingi wa mapato kwa kukusanya Shilingi bilioni 52.78 na Halmashauri ya Jiji la Tanga imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi bilioni 9.93.” ameeleza Waziri Ummy

Kwa kuongezea Waziri Ummy amesema kwa upande wa Halmashauri za Manispaa,Manispaa ya Kinondoni imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 33.25 na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi  bilioni 1. 26

Huku katika kundi la Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 6.48. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 453.72

Na. Angela Msimbira TAMISEMI

MWISHO









Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.