Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu akemea tabia ya uharibifu wa miundombinu ya barabara

Imewekwa tar.: October 19th, 2018

Mwandishi wetu, Bahi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua daraja la Chipanga na kuagiza waharibifu wa miundombinu ya barabara kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili kudhibiti tabia iliyoibuka ya baadhi ya watu kung'oa alama za barabarani.

Akizindua daraja la Chipanga wilayani Bahi akiwa ziarani wilaya humo akikagua miradi mbalimbali ya Maendeleo, Mhe Majaliwa amesema kumekuwa na tabia ya watu wasio waaminifu ya kuharibu miundombinu ya barabara na kingo za madaraja jambo ambalo linapaswa kukemewa.

Aliwataka wananchi wa Chipanga kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake lakini pia Jamii ya eneo hilo kuunda vikundi vya ulinzi ili viweze kuwakamata wahalifu hao wa miundombinu ya barabara na madaraja na kuwafikisha mahakamani.

"Kumeibuka tabia ya watu wachache wasiokuwa na nia njema,wanang'oa alama za barabarani na kingo za madaraja ,vitendo hivi vinasababisha ajali, hao ni watu wasiopenda Maendeleo watolewe taarifa,wakamatwe, wafikishwe mahakamani na tutawafunga,” alisema Waziri Mkuu.

Awali akikagua ujenzi wa nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuishi walimu sita katika shule ya sekondari Mpalanga, Mhe. Majaliwa amepongeza ujenzi wa nyumba hiyo na kuahidi kuwa serikali itaendelea kutatua kero zinazowakabili walimu huku akiagiza wilaya hiyo kujenga shule ya msingi kila Kijiji.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzindua daraja hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amesema tayari Serikali imetoa sh. billioni 2.18 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo na mkandarasi tayari ameshalipwa Sh.Bilioni 2.14.

Alisema kabla ya ujenzi wa daraja hilo, kulikuwa na athari nyingi kwa wananchi ikiwemo kukata mawasiliano baina ya wananchi wa upande mmoja na Halmashauri ya wilaya ya Bahi na hivyo kukosa huduma muhimu waliokuwa wakizihitaji ikiwemo watoto kushindwa kwenda shule.

Alisema awali wakati wa ujenzi unaanza kulikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mkandarasi kushindwa kuendana na kasi iliyotakiwa lakini baadaye walienda sawa na hatimaye daraja limezinduliwa.

Kadhalika, alisema serikali imetoa Sh.Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo Vya Afya vitatu Vya Wilaya hiyo na Sh.Bilioni 1.5 zitapelekwa Mwaka huu wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 2 May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.