Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wataalamu wa Afya endelezeni Usimamizi Shirikishi wa Afya ya Mazingira Shuleni na kwenye Jamii - Dkt Gwajima.

Imewekwa tar.: June 19th, 2020

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughukia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, amewasisitiza Maafisa Afya kote nchini kuhakikisha wanaimarisha ufuatiliaji wa uelimishaji na ukaguzi wa mazingira ya shuleni na kwenye Jamii wakiwa na wataalamu wa Sekta zingine kama Elimu ili kuimarisha afya za watanzania katika kila pahala.

Dkt. Gwajima amesema hayo akiwa na jopo la wataalamu wa Afya na Elimu walipofanya ziara ya kikazi yakutembelea na kukagua Shule za Sekondari zilizopokea wanafunzi wa kidato cha sita wanao tarajiwa kuanza mitihani yao yakuhitimu kuanzia Juni, 29, 2020 ambapo, katika ziara hiyo, Shule na Vituo vya afya vilivyofikiwa ni pamoja na Aldergate Sekondari, Babati Day Sekondari na Kituo cha Afya Mutuka, maeneo mengine ni Singe Sekondari, Bonga Sekondari pamoja na Hayatul Islamiya Sekondari.

Akiwa katika ziara hiyo, Dkt Gwajima aliridhishwa na hali ya usafi wa mazingira na huku akihoji wapi ambapo Maafisa Afya hawa huwa wanakwama katika kuendeleza ajenda ya usimamizi ili hali iwe kama ilivyo hizi siku zote?

Katika ziara hiyo, Dkt Gwajima ameshuhudia mazingira yakiwa safi na vifaa vya maji ya kunawa mikono na sabuni vikiwa kila sehemu huku vyoo na bafu vikiwa vinang’ara bila harufu yoyote kiasi cha kuweza hata kula chakula bila adha yoyote na usigundue kama hizo ni sehemu za kutunza uchafu, ameweza kushuhudia   sehemu za kulala wanafunzi, darasani na wanapopata chakula (Bwaloni) kukiwa na mpangilio mzuri na kwa nafasi isiyopungua mita moja toka mwanafunzi mmoja hadi mwingine.

Hata hivyo, Dkt. Gwajima alibaini kuwa katika baadhi ya shule kunaweza kukawa na changamoto ya nafasi iwapo wanafunzi wataongezeka hivyo, ameagiza maafisa afya wafuatilie na kuhakikisha wamiliki wa shule hizo wanaanza maandalizi mapema ya  maboresho ya mpangilio wa vitanda kwenye mabweni ili kuendelea kuepuka misongamano ya wanafunzi. Vilevile, ameelekeza kuhakikisha usafi ambao ameuona uwe uendelevu hata baada ya wanafunzi wote kurejea shuleni na kusiwe na visingizio vyote mara watoto wamekuwa wengi mara wengine wadogo kwani katika kipindi hicho ndiyo usafi huo unatakiwa kuwa bora zaidi.

Amewaelekeza Maafisa Afya kote nchini kuhakikisha ajenda ya usafi mashuleni na kwenye maeneo mengine ya jamii kuwa imara na endelevu daima ili kuimarisha zaidi udhibiti wa magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu wa mazingira na misongamano inayo epukika.

Amekumbusha kuwa, tabia ya uwepo wa misongamano ya vitanda mabwenini inahatarisha usalama wa watoto iwapo itatokea kuna dharura ya ajali na kutakiwa kujiokoa hivyo wamiliki wa shule waachane nayo mara moja na Maafisa Afya wafuatile kwa karibu na kujiridhisha hali ilivyo.

“Huu ni wakati wa kufanya mapinduzi makubwa katika utekelezaji wa ajenda ya Afya ya Usafi wa Mazingira kwa ujumla wake na kuendelea kudhibiti kila aina ya ugonjwa utokanao hali duni eneo hilo”. Amesema Dkt. Gwajima, na kuongeza, sasa hakuna sababu ya kushindwa kwani katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 chini ya uongozi wenye maono makubwa ya Kamanda wa Vita Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli Tanzania imeithibitishia Dunia kuwa tunaweza hivyo, hakuna kurudi nyuma kamwe bali kwenda mbele kutekeleza Sera na Miongozo ya Afya ya Mazingira.

Amesisitiza Maafisa Afya na Maafisa Elimu kuungana kwa pamoja katika kupunguza uhitaji wa raslimali kwa ajili ya utekelezaji endelevu mfano ni muhimu wawe na ratiba ya pamoja ya kwenda kufanya ufuatiliaji na uelimishaji kuhusu afya ya mazingira katika shule badala kila mmoja anabeba gari lake kwa ratiba yake na anafuatilia suala lile lile ambalo wote wangelifuatilia kwa pamoja kwa raslimali chache zaidi na kupata matokeo makubwa zaidi kwa muda mfupi na usiowachanganya wale wanaofanyiwa ufuatiliaji.

Dkt Gwajima ameagiza Maafisa Afya kote nchini ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuwa na Mpangokazi na Ratiba ya Ufuatiliaji na Uelimishaji kuhusu Afya ya Usafi na Mazingira kwenye Shule na Jamii na taarifa iwe inawasilishwa kila mwezi na ioneshe wazi kuwa zoezi lilikuwa shirikishi

“Mganga Mkuu wa Mkoa na Afisa Elimu Mkoa hakikisheni mnapofanya Kaguzi za Afya ya Usafi na Mazingira kwa ushirikiano ili kuendelea kudumisha usafi unao oonekana sasa na kudhibiti magonjwa yote yanayotegemea usafi duni na kuwezesha kuokoa fedha iliyokuwa ikahudumie wahanga wa magonjwa hayo na kuielekeza kwenye shughuli zingine za maendeleo.

Kuhusu suala la msongamano wa vitanda mabwenini huku vingine vikiwa havitumiki amwewataka wasimamie kwani wanafunzi wanatakiwa kulala kwa nafasi na kupata hewa safi huku wakiwa na uhakika wa kujiokoa iwapo itatokea dharura. Hivyo, huku akikemea tabia ya kujaza vitanda na masanduku kwenye korido liishe mara moja na akaagiza atumiwe picha za hali halisi ilivyo mabwenini. Vilevile, simamieni wanafunzi hawa wafunge Vyandarua na kuvitumia siyo vyote viko masandukuni kwani Mbu wa Malaria naye ni adui ambaye bado yupo.

Kwa upande wake mtaalam wa Afya Mazingira kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Selemani Yondu, alisema ugonjwa wa Corona umetufundisha kunawa mikono ili kujikinga lakini katika uhalisia sio maradhi haya tu bali pia tabia ya kunawa kwa maji tiririka na sabuni inatuepusha na maradhi mengine mengi kipindupindu na homa za matumbo na kuhara.

Naibu Katibu Mkuu akiwa katika Ziara hiyo alipotembelea kituo cha afya Mutuka, hakusita kuwapongeza wananchi wa Kijiji hicho waliojitolea nguvu zao pamoja na maeneo yao katika katika kuhakikisha ujenzi kituo cha kituo cha Afya unafanikiwa mara baada ya kupokea shilingi Mil. 200 kutoka serikalini ikiwa ni jitihada za Serikali kuwaondolea adha ya huduma za afya.

Amempongeza Mganga Mkuu wa Mji wa Babati kwa kuufahamu vema mradi huo jengo kwa jengo na chumba kwa chumba na kuwataka wataalamu wote  kuiga mfano huo ili kuepusha gharama za marekebisho ya mara kutokana na mapungufu yanayoepukika.

Naibu Katibu Mkuu alikuwepo mkoani humo kufuatilia kwa karibu masuala mazima ya Afya na Usafi wa Mazingira katika Jamii pamoja na taasisi za umma na zile za watu binafsi kama zinatekeleza ajenda ya afya kwa ufasaha.

Na. Atley Kuni –MANYARA

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.