Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wanawake washauriwa kuzingatia Lishe bora

Imewekwa tar.: December 14th, 2018

Wanawake wameshauriwa kuzingatia kanuni za ulaji wa lishe bora, mazoezi pamoja na ufanyaji wa uchunguzi wa Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi mara kwa mara ili kuweza kugundua tatizo mapema na kuweza kupata tiba badala ya kusubiri hadi madhara makubwa yajitokeze.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mshauri Idara ya Lishe na Mazoezi, Taasisi binafsi ya ‘BORABORA Self-Health Care Promotion’ kutoka nchini Japan, Tada Makiko, wakati akitoa mafunzo juu ya ugonjwa wa Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi kwa watumishi wanawake wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yaliyofanyika katika Ofisi ya Rais (TAMISEMI) leo jijini Dodoma.

Akieleza kuhusu chanzo kikubwa cha maradhi hayo ya Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi,Makiko amesema kuwa saratani ya matiti husababishwa na homoni ya kike iitwayo Estrojeni. Huku asilimia 99 ya chanzo cha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni maambukizi ya virusi vya ‘Human Papillomavirus’ (HPV) ambavyo huambukizwa kwa njia ya kujamiina haswa mwanaume anapojamiina na wanawake wengi na kisha kumletea mwenza wake maambukizi hayo.

Makiko amezungumzia pia vihatarishi vingine vya saratani ya matiti ni pamoja na unene uliozidi, kutokuzingatia lishe kamili, historia ya ugonjwa huu katika familia, Umri kuanzia miaka 45 na kuendelea, wanawake wanaobeba ujauzito kwa mara ya kwanza wakiwa katika umri wa miaka 30 na kuendelea pamoja na kutokufanya mazoezi ya mwili.

“Ni rahisi kuujua uvimbe wa tofauti kwenye matiti kwani ni laini na upo kama tezi, utaweza kuutambua baada ya siku za hedhi kwani matiti yanakuwa yamerudi katika hali ya kawaida, kama ukiacha uvimbe usambae basi saratani itasambaa kwenye mapafu, mifupa na ini hivyo kuhusababishia maumivu makali na hata kifo” alisema Makiko.

Akiongezea kuhusu masuala hayo ya saratani, Makiko alisema kuwa asilimia 80 ya wanawake walioathiriwa na saratani hii hufariki dunia nchini Tanzania kutokana na kuchelewa kufika hospitali kwa ajili ya kupata matibabu kabla ya tatizo kuwa kubwa ingali kuwa huduma hiyo hutolewa bure katika vituo vya afya na hospitali.

Dalili za kuonyesha kwamba saratani ya matiti imesambaa mwilini ni pamoja na kushindwa kupumua vizuri iwapo imesambaa kwenye mapafu,maumivu makali ya mifupa iwapo imesambaa kwenye mifupa na kusababisha mwili kuwa wa manjano,kichefuchefu na kutapika iwapo imeenea kwenye ini, pia kutokwa na damu baada kujamiina hii ni dalili ya saratani ya shingo ya kizazi, Alisema Makiko.

Akichangia umuhimu wa kuzingatia mazoezi, lishe pamoja na kuwahi kupata matibabu mmoja wa waliohudhuria mafunzo hayo ambaye pia ni Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu alimshukuru mtaalamu huyo kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani pia ni mmoja wa wanufaika wa huduma zitolewazo na Taasisi ya ‘BORABORA Self-Health Care Promotion’.

“Nimehudhuria mazoezi yanayotolewa na taasisi hii, ni mazuri na sio magumu kuweza kufuatilia na faida zake ninaziona kwangu.” Alisema Kwandu.

Ni muhimu kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi mara moja kwa kila baada ya miaka miwili au mitatu, pia kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti mara moja kwa mwezi kwa wanawake ambao bado hupata siku za hedhi na kwa waliokoma kupata hedhi kuweza kufanya wakati wowote uchunguzi wa saratani hio.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.