Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wanafunzi Simiyu wawatahadharisha Wasimamizi wa Mitihani 2018

Imewekwa tar.: August 28th, 2018

Wanafunzi wa darasa la saba kutoka shule za msingi za Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu wamemuomba Mkuu wa Mkoa, Mhe Anthony Mtaka, kuwataka  wasimamizi wa Mtihani wa Taifa wenye tabia ya kuwatisha wanafunzi wakiwa katika chumba cha mtihani waache tabia hiyo ili wanafunzi wafanye Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, mwaka 2018 kwa uhuru pasipo uoga.

Wanafunzi hao wametoa ombi hilo Agosti 27, 2018, mbele ya Mkuu wa Mkoa wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipokutana na wanafunzi wa darasa la saba takribani 782 wa shule tano za msingi za Mjini BARIADI, katika Shule ya Msingi Sima B, lengo likiwa ni kuwaandaa na kuwahimiza kusoma kwa bidii katika siku chache zilizobakia na kuwatakiwa kila la heri katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.

Wamesema kuwa wamepata taarifa kutoka kwa wenzao waliowatangulia kuwa siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba ambao walikuwa wakiwatisha na kuwanyanyasa watahiniwa, hivyo kuwafanya wanafunzi kufanya mtihani wakiwa na hofu jambo lililofanya baadhi yao kushindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

“Miaka ya nyuma tunasikia kuna wasimamizi walikuwa wanawatishia sana wanafunzi, tunaomba  Mkuu wa mkoa utusaidie na sisi wasije wakatutishia tukashindwa kufanya mtihani wetu wa Taifa vizuri” alisema John Isack Mwanafunzi wa darasa la Saba Shule ya Msingi Sima A, Bariadi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wanafunzi hao kuwa hakutakuwa na vitisho wala manyanyaso yoyote kutoka kwa wasimamizi wa mitihani na akawaeleza kuwa atakutana na wasimamizi wa mitihani ambao wapo katika semina elekezi na  kuwapa angalizo hilo.

“Nikitoka hapa sasa hivi naenda kuongea na wasimamizi wa mitihani, niwahakikishie tu kwamba hamtatishwa msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni kujisomea mjiandae vizuri na mtihani na mkiwa kwenye chumba cha mtihani mkawe watulivu na kumwomba Mungu awakumbushe yote mliyokuwa mnajisomea” alisema Mtaka.

Akizungumza na wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba, Mtaka amewataka wasimamizi hao ambao ni walimu kuwasimamia wanafunzi hao huku wakitambua kuwa wao ni walezi, hivyo wanapaswa kusimamia kwa kufuata taratibu zilizowekwa pasipo kuwatisha wala kuwanyanyasa watahiniwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa mwanafunzi wa kiume, milioni moja na laki tano kwa mwanafunzi wa kike atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka 2018 na shilingi milioni tatu kwa Shule ya Msingi ya Mkoa huo itakayokuwa miongoni mwa shule kumi bora Kitaifa.

Nao wanafunzi wa Darasa la Saba Mjini Bariadi wamemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watafanya vizuri katika Mtihani wa Taifa kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao katika shule zao na katika kambi za Kitaaluma walizokaa kwa siku 21 mwezi Juni kujiandaa na mtihani huo.

“Tunakushukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kutuwezesha kuwa na kambi za kitaaluma, zimetusaidia kutuandaa na mtihani wa Taifa maana tulijifunza vitu vingi, tukapata maarifa mapya, sasa pia hivi walimu wetu wametuandaa vizuri tuko tayari kwa Mtihani wa Taifa, tunakuahidi tutafanya vizuri” alisema Hilda Mgalula Mwanafunzi wa darasa la saba Sima B.

Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime amesema jumla ya watahiniwa elfu 35 Mkoani Simiyu wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la saba Septemba tano na sita, mwaka 2018.

Anaandika, Stella Kalinga Kutoka Simiyu.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.