Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wanafunzi 4,105 wachaguliwa awamu ya pili kujiunga na kidato cha tano mwaka 2021

Imewekwa tar.: August 16th, 2021

Wanafunzi 4,105 wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa mwaka huu katika uchaguzi wa awamu ya pili kutokana na waliochaguliwa awamu ya kwanza kutoripoti kwenye shule walizopangiwa.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Prof.Riziki Shemdoe, wakati akitangaza  matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili mbele ya waandishi wa habari  jijini Dodoma.

Prof. Shemdoe amesema kuwa kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 499 (wavulana 424 na wasichana 75) wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 3,604 wakiwemo wavulana 3,461 na wasichana  143 wamepangiwa tahasusi za masomo ya Sanaa na Biashara.


Amebainisha kuwa upangaji wa awamu ya pili umefanyika baada ya Wizara kujiridhisha na nafasi zilizo wazi  katika shule ambazo wanafunzi hawakuripoti.


“ Kwa kuangalia idadi ya wasichana waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili imekuwa ndogo, hii ni  kwa sababu katika uchaguzi wa awamu ya kwanza wanafunzi wote wasichana waliokuwa na vigezo walichaguliwa hivyo hapakuwa na wanafunzi wasichana  waliokuwa wamebakia,”amesema Prof. Shemdoe


Amefafanua kuwa wanafunzi wasichana waliochaguliwa katika  awamu ya pili ni wale ambao waliomba kubadilishiwa machaguo yao kutoka vyuo mbalimbali walivyokuwa wamechaguliwa awali na kupelekwa kidato cha tano.


“Wanafunzi waliopangwa awamu ya pili wanatakiwa kuripoti katika Shule walizopangiwa kuanzia leo tarehe 16 hadi 30 Agosti, 2021, hivyo mwanafunzi ambaye atashindwa kuripoti hadi tarehe 30 Agosti, 2021 atakuwa amepoteza nafasi yake,”amesisitiza Prof . Shemdoe.

Aidha, amewaomba wazazi na walezi waelewe kwamba hakutakuwa na nafasi yoyote ya wanafunzi hawa kubadilishiwa shule kwa kuwa shule walizopangwa ni zile zilizobainika kuwa na nafasi kwa tahasusi husika.




Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.