• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Wafugaji nchini watakiwa kuunda vyama vya ushirika

Imewekwa tar.: June 4th, 2018

Angella Msimbira-OR TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege  amewaagiza wafugaji nchini kuunda  vyama vya ushirika imara ambavyo vitawezesha  kupata huduma za mifugo na kuboresha ukusanyaji na masoko ya maziwa.

Mhe Kandege ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maziwa iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nanenane, Themi Mkoani Arusha

Mhe. Kandege amesema uwepo wa ushirika imara utaboresha ukusanyaji wa  maziwa kwa wingi kwa ufanisi zaidi na hatimaye  kuongeza kiasi cha usindikaji kwa viwanda.

“Napenda kutoa pongezi kwa wafugaji wa Mikoa ya Tanga na Njombe kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika” Amesema Kandege

Amesisistiza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na idara zake nchini kuhakikisha zinawezesha uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia wanaimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.

“Mtambue kuwa kuwepo kwa ushirika imara kunaweza kutatua changamoto nyingi. uwezo wa viwanda vya kusindika maziwa hapa nchini bado ni mdogo ukilinganisha na uwezo halisi wa viwanda hivyo”. Amesema Kandege

Mhe. Kandege ametoa rai kwa wadau wa sekta binafsi kujitokeza kwenye maonesho ya wafugaji kwa malengo ya kuongeza tija na kuimarisha viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo kwa kuwa  Serikali itaendelea kutoa msukumo wa pekee katika kuendeleza ufugaji wa kisasa nchini na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya tasnia ya maziwa wanaendelea kukamilisha mchakato wa  kuandaa mpango kabambe wa kuendeleza mifugo ambao unahusisha pia tasnia ya maziwa nchini.

Amewataka wadau wengine kuwekeza katika kujenga na kuendesha viwanda vya maziwa hapa nchini ili kuongeza uwezo wa kuzalisha zaidi bidhaa ambazo ni bora na zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya soko.

Kuhusu uhaba wa ng’ombe wa maziwa Mhe Kandege Serikali imeandaa mpango kabambe wa kuhakisha upatikanaji wa ngo’mbe bora wa maziwa kwa kuzalisha ndama milioni moja wa ng’ombe wa maziwa kila mwaka na  TAMISEMI na Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za uhimilishaji na upatikanaji wa gesi ya nitrojeni kwa kukiimarisha kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) na vituo vya Kanda na ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe. Kandege amesema Wafugaji wanapaswa kuboresha mbinu zao za uzalishaji kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa. Na muhimu zaidi wafugaji waunde vyama vya ushirika ambavyo vitaongeza tija katika upatikanaji wa pembejeo, huduma za ugani na huduma za kifedha.

Amesema vyama ya ushirika vitakuwa kitovu cha upatikanaji wa huduma na masoko ya maziwa wanayozalisha. Wasindikaji pia waendelee kukusanya maziwa yanayozalishwa kutoka kwa wafugaji na kuyanunua kwa bei nzuri ili kutoa motisha kwa uzalishaji zaidi wa maziwa na kuyasindika.

Mhe Kadege  amewaagiza Mameya/ Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wote na wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanahudhuria  bila kukosa katika maonesho yajayo ambayo Kimataifa yatafanyika Jijini Arusha ili waweze kujifunza  na kwenda kutoa elimu kwenye Halmashauri zao.

Aidha Katika hatua nyingine Mhe. Kandege alishiriki zoezi la ugawaji  wa maziwa kutoka  kampuni ya Asas ya Iringa katika shule za msingi Terrati, Madosoita,Suye, Losiyo,Nkonoo, Osunyai na Kimandolo zilizoko Mkoani Arusha.




Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.