Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wadau wakutana kujadili Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Imewekwa tar.: April 1st, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo wamewataka viongozi na wawakilishi vya vyama vya siasa kuhakikisha wanatoa maoni yenye tija ili kutengeneza kanuni zilizo bora zitakazo simamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha, Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika muda wote kati ya Novemba au Desemba mwaka huu.

Jafo aliyasema hayo wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili uliokutanisha vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambao wana kazi ya kujadili rasimu ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika baadaye mwaka huu.

Alisema Tanzania inaongozwa kwa utaratibu wa demokrasia, hivyo Serikali ilioana kutengeneza  jukwaa la kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo vyama vya saisa ili kuwa na kanuni bora zitakazoendesha uchaguzi kwa amani na utulivu.

“ Nikiwa nimepewa mamlaka hii na Rais John Magufuli, nikaona sio vyema kwa mujibu wa utaratibu wa undwaji wa kanuni hizi lazima tuunde kanuni ambazo zinamchango mkubwa wa wadau mbalimbali ambao utasaidia sana katika mwenendo wa uchaguzi tunaoendana nao

“Tunapokea maoni kutoka kwa wadau, na kundi hili ambalo linawakilisha vyama vya siasa vyenye usajili  ni muhimu sana kwasababu ndio kundi ambalo linachakata kwa muda wote katuni hizi na wenye wajibu wa kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali.

Alisema kutokana na umuhimu wa vyama vya siasa katika uundwaji wa kanuni za uchaguzi, ofisi yake ilipeleka rasimu hiyo mapema kwa wadau ili kuweza kupata muda wa kupitia na kuja na maoni yaliyobora.

“Ndio maana nimewapa maelekezo ni vyema kanuni kuwafikia wadau siku chache kabla hatujakutana wapate muda wa kuzipitia ili kupata maoni mazuri.

Aliongeza: “ Wakati mwingine tukipeana kanuni ukumbini, inakuwa sio jambo jema sana na inakuwa kama ni jambo la kuviziana, hili ni jambo letu sote kwa ajili ya nchi yetu, mapema kupata ushauri mzuri ulio bora na kanuni ziwe nzuri na imara ili kuweza kushiriki uchaguzi za serikali za mitaa kwa uzuri.

Jafo alisema kanuni hizo zinamaeneo matatu ikiwa ni pamoja na Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji katika mamlaka ya serikali za mitaa za mwaka 2019.

Alisema pia kuna Rasimu ya uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa, na wajumbe wa kamati ya mtaa katika mamlaka ya miji za mwaka 2019 na Rasimu ya kanuni ya uchaguzi wa mwenyekiti  wa kitongozi katika mamlaka za miji midogo za mwaka  2019.

“ Nimatumiani yangu tutatumia muda vizuri katika kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni na michango mbalimbali kusaidia kuboresha rasimu za kanuni kwa lengo la kukuza demokrasia hapa nchini na utawala bora.

“ Taifa letu ni taifa la mfano, pengine mataifa mengine hayapati jukwaa kama hii la kuweza kubadilishana mawazo hivyo kuzidi kuimarisha demokrasia,” alisema.

Aliongeza: “ Ni imani yangu mchakato utaenda vizuri na utakuwa wenye tija kwa wajumbe kutoa maoni bora ili mwisho wa siku shiriki Novemba au mwishoni wa mwaka huu kwa jinsi Mungu atakapotupa kibari.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa, John Shibuda alisema watahakikisha wanatengeneza kanuni zitakazojenga taswira nzuri ya nchi Kitaifa na Kimataifa.

Aliomba katika kikao hicho Msajili wa vyama atoe uwianishaji wa kanuni hizo pamoja na Sheria mpya ya vyama vya siasa ili isijeleta msuguano wakati wa uchaguzi huo.

“Ili kuondokana na dukuduku na sintofahamu kuwepo uwianishaji wa sheria ya vyama vya siasa na kanuni hizi za uchaguzi, tuongeze muda wa majadiliano uwe siku tatu ili tumsikie msajili anasemaje kwenye hili ili isitokee misuguano,”alisema.

Pia Shibuda alipongeza juhudi za Rais John Magufuli za kuimarisha uchumi wa nchini na kuwa wao kama vyama siasa hawana upogu wa macho na akili wa kutambua juhudi hizo.

Jana wajumbe walipitishwa katika rasimu hiyo na watatumia siku ya leo kufanya majadiliano na kesho itakuwa zamu ya asasi za kiraia kutoa maoni yake.

Baadhi ya vyama vilivyotuma wawakilishi ni Chama cha Mapinduzi(CCM), Chama cha Wananchi(CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ARA, Union for Multiparty Democracy(UMD), ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, National League For Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party(UPDP), National Reconstruction Alliance(NRA) na Tanzania Democratic Alliance(TADEA).

Tanzania Labour Party(TLP), United Democratic Party(UDP), Demokrasia Makini (MAKINI), Democratic Party(DP), Sauti ya Umma(SAU), Tanzania Farmers Party(AFP), Chama cha Kijamii(CCK), Alliance for Democratic Change(ADC) na Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA).



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.