• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Timu za Uhamiaji, na Mgulani JKT zasalimu amri kwa TAMISEMI QUEENS

Imewekwa tar.: July 26th, 2021

Na Mathew Kwembe, Arusha

Timu za Netiboli za JKT Mgulani na Uhamiaji zote kutoka jijini Dar es salaam jana zilipoteza michezo yake ya Ligi daraja la kwanza baada ya kukubali kipigo kutoka kwa TAMISEMI QUEENS ambao ni Mabingwa wa Kombe la Netiboli la Muungano mwaka 2019, katika mchezo mkali na wa kusisimua uliochezwa jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ya jijini Arusha.

Timu ya JKT Mgulani ndiyo ilikuwa ya kwanza kukumbana na kipigo kutoka kwa TAMISEMI QUEENS baada ya kupoteza mchezo wake kwa kufungwa magoli 46-32.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi wa netiboli hadi robo ya kwanza inamalizika TAMISEMI QUEENS walikuwa wanaongoza kwa magoli 18-3.

Katika robo ya pili na ya tatu TAMISEMI QUEENS walikuwa mbele kwa magoli 30-10, na baadaye 40-19 na hadi mchezo unamalizika katika robo ya nne na ya mwisho, TAMISEMI QUEENS walishinda mchezo huo kwa magoli 46-32.

Katika mchezo huo mkali uliochezwa asubuhi, TAMISEMI QUEENS walilazimika kuwapumzisha baadhi ya nyota wake kama vile Sophia Komba, anayecheza eneo la katikati, Golikipa Chuki Kikalao na Mlinzi Mersiana Kizenga kwani timu hiyo ilikuwa na mchezo mwingine mgumu dhidi ya uhamiaji mchana.

Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Mshambuliaji wa pembeni wa timu hiyo Lilian Jovin ambaye alionyesha umahiri mkubwa wa kufunga magoli kila mara alipolikaribia goli la JKT Mgulani.

Katika mchezo mwingine kati ya TAMISEMI QUEENS dhidi ya Uhamiaji ya Dar es salaam ambao ulichezwa jana jioni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, hadi mwisho wa mchezo TAMISEMI QUEENS ilifanikiwa kuilaza Uhamiaji magoli 49-31.

Timu zote mbili zilionyesha nia ya kushinda mchezo huo kwani hadi robo ya kwanza ya mchezo inamalizika, timu hizo zilitoka sara kwa kufungana magoli 9-9.

Mambo yalibadilika katika robo ya pili na ya tatu kwani wachezaji wa TAMISEMI QUEENS mara kwa mara walikaribia goli la Uhamiaji na kufanikiwa kutumbukiza mipira 23 dhidi ya 14 ya uhamiaji na katika robo ya tatu TAMISEMI QUEENS walifanikiwa kutumbukiza mipira 35 dhidi ya 20 ya Uhamiaji.

Katika robo ya mwisho, wachezaji kutoka timu zote mbili walionekana kuchoka, na hivyo kupunguza kasi ya mchezo huo mkali na wa kusisimua lakini hata hivyo timu ya TAMISEMI QUEENS ilifanikiwa kuongeza magoli mengine baada kumuongeza mchezaji wake mkongwe Aziza Itonye (GA) ambaye mara kwa mara alifanikiwa kurusha mpira ndani ya goli la uhamiaji.

Magoli ya TAMISEMI QUEENS katika mchezo dhidi ya Uhamiaji yalifungwa na Lilian Jovin, na Aziza Itonye  na kwa upande wa Uhamiaji magoli yalifungwa na Fatuma Machenga na Matalena Mhagama.

Timu hiyo ya TAMISEMI QUEENS ambayo ndiyo timu pekee inayotoka katika Wizara za kiserikali kwa sasa imebakiza michezo miwili ambayo ni dhidi ya Eagles Queens na Mbweni JKT zote za jijini Dar es salaam huku, mchezo wao dhidi ya Mbweni JKT utahitimisha mashindano haya tarehe 29 julai 2021

Naye, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya TAMISEMI Philbert Rwakilomba amesema timu yake imekuja hapa Arusha kupambana ili ibebe kombe la ligi daraja la kwanza mwaka huu.

Amesema timu yake ilijiandaa vizuri kushiriki mashindano hayo na akawapongeza Viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuiwezesha timu yake kufanya maandalizi mazuri na hatimaye kushiriki mashindano hayo.

Rwakilomba pia amewapongeza waandaji wa mashindano hayo Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa mapokezi mazuri ambayo timu yake imeyapata na pia amekipongeza Chama cha mchezo wa Netiboli Tanzania CHANETA kwa kusimamia kanuni na taratibu za mashindano hayo.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Benson Maneno ameishukuru CHANETA kwa kukubali mashindano ya Ligi daraja la kwanza Netiboli kufanyika Arusha mwaka huu, na ameahidi kutafuta wadhamini zaidi ili mashindano hayo yatakapofanyika tena Arusha hapo  mwakani washindi waweze kupata zawadi nono zaidi.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.