Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TAMISEMI yajivunia mafanikio makubwa ndani ya miaka minne

Imewekwa tar.: February 4th, 2020

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI), imetaja mafanikio sita yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne huku ikisema tatizo la usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaotumia mabasi ya mwendokasi itamalizika Julai mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni wiki na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo,wakati alipokuwa akizungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, Jijini Dodoma.

Ametaja mafanikio hayo kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya barabara, Hospitali za wilaya na vituo vya afya, Mpango wa elimu bure, ukusanyaji mapato, ujenzi wa viwanda vidogo, utoaji mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ujenzi wa miradi mikakati, ujenzi wa miundombinu ya barabara  na mradi wa mabasi yaendayo kasi.

Mhe. Jafo amesema ujenzi wa miundombinu ya barabara unaofanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(Tarura) umekuwa na mafanikio makubwa na kurahisisha usafiri kwa wananchi.

Amebainisha kuwa katika eneo hilo, kumekuwepo na miradi ya kimkakati kwa majiji na manispaa ambapo zaidi ya Sh.Bilioni 840 zinatumika kujenga barabara, masoko, stendi za kisasa, mitambo na madampo ya taka.

Akizungumzia sekta ya afya, amesema kabla ya uongozi wa Rais Magufuli kulikuwa na vituo vya afya 115 lakini serikali imejenga vituo 352 ambavyo vina uwezo wa kufanya upasuaji.

“Pia zimejengwa hospitali za wilaya 69 na mwaka huu wa fedha zitajengwa zingine 27 kwa kupitia utaratibu wa ‘force account’,”Amesema Mhe. Jafo.

Kuhusu sekta ya elimu, Jafo amesema  kila mwezi serikali inatoa Sh.Bilioni 23.86 kugharamia elimu bila malipo.

“Pia tumeboresha shule kongwe ambazo zilikuwa zimechakaa na kwa wastani wa Sh.Milioni 800 hadi Sh.Bilioni 2 kwa kila shule zinatumika kukarabati,pia miundombinu ya shule za msingi na sekondari imejengwa na inaendelea kujengwa,”amesema

Kadhalika, amesema tayari  Serikali imeweka sheria kwa ajili ya utoaji mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo asilimia 10 ya mapato ya ndani yanatumika kwa ajili hiyo na mabilioni ya fedha yametolewa kwa makundi hayo.

Mhe. Jafo amesema kwenye ujenzi wa viwanda vidogo, lengo lilikuwa kila mkoa kuwa ni viwanda 100 lakini hadi kufikia Desemba 2018 viwanda 4,877 sawa na asilimia 186.75 vilikuwa vimejengwa.

Akizungumzia ukusanyaji wa mapato, amesema serikali imeanzisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki  ambapo kumeleta mapinduzi makubwa kwenye makusanyo na kuwepo na uadilifu.

Kuhusu Mabasi yaendayo kasi Mhe Jafo amesema tatizo la usafiri kwa wananchi litamalizika baada ya mzabuni mpya wa kuendesha mradi kupatikana.

“Shida inayojitokeza sasa ni upungufu wa mabasi ambapo yanayofanyakazi ni 140 kati ya mabasi 305 yanayohitajika, mzabuni mpya ataleta mabasi yote 305 yanayohitajika kutoa huduma ya usafiri,”amesema

Amesema  ifikapo Julai hadi Agosti mwaka huu, shida hiyo itamalizika baada ya serikali kumpata mzabuni huyo huku akisema awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi huo kwenda Mbagala imekwishaanza, na itafuatiwa na awamu ya tatu kwa ajili ya mabasi ya mwendokasi kuelekea Gongo la Mboto.

Aidha ,amesema kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu Jiji la Dar es Salaam (DMDP) barabara za mitaa zinazojengwa zitakuwa kiungo muhimu na zile za mwendokasi.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.