• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali yaliridhishwa na ujenzi wa madarasa mapya ya sekondari

Imewekwa tar.: November 26th, 2021

Na Fred Kibano, Lindi

Serikali imepongeza kasi ya ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza 2022 yanayoendelea kujengwa mkoani Lindi licha ya kuwa katika hatua tofauti tofauti za ujenzi

Hayo yamesemwa na Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI alipofanya ziara yake ya kikazi hii leo wilayani Kilwa mkoani Lindi ambapo amejionea kasi ya ujenzi na uwepo wa vifaa vyote muhimu kwa hatua zote zilizobaki na kwamba dhamira ya Serikali ya kuamua kutokuwa na machaguo zaidi ya mawili mwaka 2022 kufikiwa.

Dkt. Dugange amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa pekee imepokea kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni mia sita kwa ajili ya kujenga madarasa 74 ya sekondari na madrarasa 29 ya shule shuikizi ambayo yote yatatumika katika kipindi cha kuanzia mwezi januari, 2022.

“dhamira ya Serikali ni kuhakikisha watoto wetu wote ifikapo januari 2022 wanaingia darasani siku moja, bila kuwa na chaguo la kwanza, chaguo la pili na chaguo la tatu ambazo mara nyingi yale machaguo zilikuwa zinachangiwa na uhaba wa madarasa au ufinyu wa madarasa, tulikuwa na utaratibu wa kunajenga madarasa kwa zimamoto muda wa watoto kuingia darasani unafika madarasa hayajakamilika, na ndio maana Serikali sasa imedhamiria kuhakikisha inapofika tarehe ya kufungua shule kidato cha kwanza watoto wetiu wote wa sekondari wanaaza siku moja masomo yao ya kidato cha kwanza”

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bw. Shaibu Ndemanga amesema Wadau wote muhimu wameshirikishwa wakiwemo Madiwani, Wakuu wa shule, watendaji wa kata na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya na matarajio kuwa ujenzi wa madarasa utakamilika mapema tarehe 15 desemaba, 2022.

Dkt. Dugange amesema utekelezaji wa ujenzi huo utaweza kufikia malengo ya Serikali endapo tarehe iliyowekwa kitaifa ya kukamilisha ujenzi itazingatiwa na Halmashauri zote ambayo ni tarehe 15 desemba maka huu kwa kuongeza kasi zaidi na hata kujenga usiku na mchana.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya sekondari Kilwa Jason Kashaija amesema shule yake ilipokea kiasi cha shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vine vya na watarajia kumaliza ujenzi mapema ifikapo tarehe 15 Desemba na kwamba vifaa vyote vinavyohitajika kwa hatua za umaliziaji vyote vimekwisha nunuliwa

Aidha, Kashaija amesema ujenzi mapaka sasa umegharimu ni shilingi milioni 24,611,000 na kati ya fedha hizo milioni 2,800,000 zimetumika kuwalipa mafundi lakini pia wanakabiliwa na changamoto za wananchi kutokuwa tayari kujitolea nguvu zao baada ya kusikia Serikali imetoa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa madarasa ya shule hiyo pamoja na  bei ya vifaa vya ujenzi kuwa ghali wilayani Kilwa na hivyo kupelekea kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya wilaya hiyo.


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.