Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali ya Poland yaonyesha nia ya kuisaidia Sekta ya Afya Nchini

Imewekwa tar.: May 28th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameishukuru Serikali ya Poland kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuisadia Tanzania katika Sekta ya Afya Nchini ili kuboresha na kupunguza changamoto katika Sekta hiyo.

Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka Poland cha kujadili masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini.

Mhe. Jafo ameishukuru Serikali ya Poland  kwa ushirikiano wanatoa  katika Miradi mbalimbali ya maendeleo  na kutambua  umuhimu wa sekta ya afya nchini  kwa kuwa bila kuimarisha Sekta ya afya hakutakuwa na maendeleo na kushindwa kufikia uchumi wa kati.

“Sekta ya afya ni muhimu kwa jamii, jamii isipokuwa na afya bora hakutakuwa na maendeleo, hivyo ni vyema Serikali ikajikita kuwekeza katika Sekta ya afya kwa kuhakikisha inajenga miundombinu bora, uwepo wa vifaa na vifaa tiba ili kuboresha huduma za afya nchini” Amesema Mhe. Jafo

Amesema kuwa  hatuwezi kufikia uchumi wa kati endapo watu  wetu hawatakuwa na afya bora, ili watu wafanyekazi kwa bidi waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa wanatakiwa kuwa na afya bora hivyo tunawakaribisha wadau mbalimbali wa Sekta ya afya kuwekeza katika Sekta hiyo.

Mhe. Jafo amendelea kuishukuru Serikali ya Poland kwa kuonyesha nia ya kuisaidia Serikali mkopo wenye gharama nafuu utakaosaidia kuimarisha na kuboresha sekta ya Afya nchini lengo likiwa ni kupunguza changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.

Ameiomba Serikali ya Poland kujikita zaidi katika kusaidia kwenye kuimarisha huduma za msingi hasa ujenzi wa Vituo vya afya na upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba  kwa kuwa ndipo kwenye changamoto kubwa  katika suala zima la utoaji wa huduma na itasaidia kupunguza vifo kwa jamii

Mhe. Jafo amefafanua kuwa katika eneo la Sekta ya Afya Serikali itapata fursa ya kusaidiwa ujenzi wa Vituo vya afya, ambavyo vitakuwa vya mfano kwa kuwa na vifaa vyake  na kuwa na nyumba zaidi ya nne za madaktari  na hivyo kupunguza changamoto zilizopo.

Mhe. Jafo amelishukuru shirika la Light For Africa kwa kuunganisha nchi ya Poland na Tanzania   ambao wameonyesha nia ya dhati katika kusaidia masuala ya Sekta ya Afya nchini jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa jamii

Aidha Wadau hao  watatembelea, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya Mirembe, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,  Hospitali ya Amana  na Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuangalia ni namna Tanzania inavyotoa huduma  za  afya na kuangalia maeneo ambayo wanaweza kusaidia katika kutumia fursa walizonazo.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI




Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.