Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka Kuipaisha Sekta ya Uvuvi nchini

Imewekwa tar.: September 27th, 2022

Na Fred Kibano, Dodoma

Ushirikiano wa kisekta baina ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Mifugo na Uvuvi utasaidia kuongeza mazao ya Sekta ya Uvuvi na kuinua uchumi wa wananchi wanaotegemea mazao ya Uvuvi.

Hayo yamesemwa na Bi. Beatrice Kimoleta, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi na Wataalam kilichofanyika kati ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Jijini Dodoma mapema leo.

Bi. Kimoleta amesema lengo la kikao kazi hicho ni kutekeleza maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Wizara hizo ambao waliwaeleza wataalam kukaa na kuweka mikakati ili kuwa na usimamizi wa pamoja wa Sekta ya Uvuvi kwa kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye mapato ya Serikali, kukuza uchumi na kipato cha Wananchi kwenye maeneo wanayojishughulisha na shughuli za uvuvi.

Aliendelea kueleza kuwa lengo pia ni kuhakikisha Mipango inayoandaliwa na Wizara hizi mbili inakuwa shirikishi na inayolenga kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Naye Mhandisi Enock Nyanda Mkurugenzi Msaidizi wa Sekta za Uchumi na Uzalishaji, Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema maazimio ya kikao kazi hicho yataisaidia  Ofisi ya Rais TAMISEMI  ambaye ni mtekelezaji  wa Sera kwenye Mikoa na Halmashauri na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni mtunga Sera kuona namna ambavyo mikopo ya asilimia 10 inavyoweza kutumika kuunda vikundi vitakavyojishughulisha na shughuli Uvuvi katika Halmashauri ili kuongeza tija ya Mikopo hiyo, kukuza ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo husika.

Kwa upande wake Antony Dadu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ugani wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji amesema Serikali inatarajia kununua boti 160 na kuwapatia wavuvi nchini kama Mpango wake wa kukuza Sekta hiyo. Amesema kuwa boti hizo ziendazo kasi zitakuwa na ukubwa tofauti wa mita 14, mita 12 na mita 10, pia kifaa cha kutambua samaki walipo, kasha la kuhifadhia samaki hadi tani moja na nusu, makoti ya kujiokoa na zana za kuvulia.

Aidha, amesema boti hizo zitapelekwa kwenye maeneo ya kimkakati ambayo yana kina kirefu cha maji na hali ya hewa inayowasumbua wavuvi.

Akifunga, Kikao hicho  Prof Mohamed Sheikh Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Huduma kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ameeleza kuwa ushirikiano wa karibu wa Wizara hizi utasaidia Mikakati ya kuleta Mapinduzi ya Sekta ya Uvuvi kufikiwa kwa haraka ambayo  ni pamoja na Ujenzi wa miundombinu ya uvuvi kama mabwawa, ujenzi wa mashamba darasa kuwezesha ufugaji wa samaki kwenye vizimba, mafunzo kwa wakulima wa mwani, ujenzi wa masoko ya kimkakati, ununuzi wa boti na kusimamia miradi ambayo imebuniwa na Halmashauri katika asilimia 5 fedha wanazopaswa kutenga kutoka katika mapato yatokanayo na shughuli za uvuvi.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa kukubaliana kuhakikisha uandaaji wa Mipango na Bajeti ya Halmashauri katika sekta ya Uvuvi unakuwa wa kimkakati ili kuongeza mapato na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo husika.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.