Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Sera Mpya ya Ugatuaji wa Madaraka kurahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi

Imewekwa tar.: April 1st, 2019

Na Mathew Kwembe, Mbeya

Serikali imesema kuwa Sera Mpya ya Ugatuaji wa Madaraka inalenga kuwezesha raslimali zake zishuke moja kwa moja kwenye halmashauri na vituo vya kutolea huduma kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 kwa wananchi wa mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe leo jijini Mbeya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Kisekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Juma Idd amesema kuwa rasimu ya sera hiyo imejielekeza moja kwa moja kwao kwa sababu ndiyo wanaoelewa mahitaji ya msingi ya maeneo yao.

Amesema ili kuwezesha utoaji huduma kwa wananchi kwa ufanisi, sera mpya ya ugatuaji wa madaraka imebainisha majukumu kwa kila taasisi ambapo Wizara za kisekta zitakuwa na jukumu la kutafuta raslimali, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itaendelea na jukumu la uratibu na usimamizi wa raslimali hizo na kuhakikisha kuwa zinashuka moja kwa moja katika ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vituo vya kutolea huduma za afya.

Bwana Idd amesema kuwa, kwa kufanya hivyo, wananchi waliopo kwenye vituo vya kutolea huduma wataweza kupanga, kusimamia utekelezaji wa raslimali hizo na kuzitolea taarifa.

Mkurugenzi Idd ameongeza kuwa rasimu ya sera mpya ya Ugatuaji wa Madaraka inalenga kuboresha sera ya sasa ya Ugatuaji wa Madaraka ambayo ilitayarishwa mwaka 1998 ili iweze kuendana na mazingira ya sasa ya utendaji kazi katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Mfano mzuri wa rasimu hii ni kuona sekta za afya na elimu ambapo wizara husika zimepeleka raslimali za kutosha, ngazi za halmashauri na vituo vya kutolea huduma na matokeo yake ni uboreshwaji mkubwa wa huduma za afya na elimu katika maeneo mengi nchini,”amesema.

Amesema kuwa serikali imeona ni vema viongozi hao wa Mamlaka za Serikali za Mitaa washiriki kwenye kutoa maoni kuhusu rasimu hii ya Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwani ni vizuri kwanza waifahamu rasimu yenyewe lakini pia waweze kuiboresha endapo ina mapungufu na kuondoa vitu ambavyo hawavihitaji kuwemo kwenye sera hiyo.

Mapema akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Mheshimiwa Paul Ntiniki ametaja mafanikio na changamoto mbalimbali  za utekelezaji wa ugatuaji madaraka katika kipindi kilichopita ambapo ameeleza kuwa mafanikio na changamoto hizo zinatofautiana kwenye maeneo tofauti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

“Kwa ujumla wake, hatujafikia kiwango cha mafanikio kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza na ndio maana Serikali yetu imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ugatuaji ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza,” ameeleza

Mhe.Ntiniki ameelezea matarajio yake kuona kwamba ushauri, maoni na mapendekezo ya washiriki yataboresha Rasimu ya awali ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka itakayowasilishwa na wataalam Washauri.

“Maoni na mapendekezo yenu ni muhimu sana katika kuandaa Sera mpya itakayoboresha utekelezaji wa ugatuaji madaraka nchini kwa ufanisi zaidi na kwa maendeleo ya wananchi wetu,” amesema.

Kikao hicho  cha siku mbili kimewahusisha Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa dini na Washiriki kutoka Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.