• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Nzunda ataka Halmashauri ziimarishe vitengo vya ukaguzi wa ndani

Imewekwa tar.: March 19th, 2019

Na Majid Abdulkarim na Mathew Kwembe

Serikali imewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha uwezo wa ofisi za Wakaguzi wa ndani ili waweze kusaidia jukumu la usimamizi thabiti wa fedha za umma.

Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Tixon Nzunda katika Chuo cha Serikali cha Serikali za Mitaa Hombolo kilichopo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupokea na kuhakiki taarifa za majibu na mipango kazi ya utekelezaji wa hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Bwana Nzunda amesema kuwa ni wajibu wa Wakurugenzi wa Halmashauri kama Maafisa Masuuli kuhakikisha kuwa wanaimarisha ofisi za wakaguzi wa ndani kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi, kuwapa raslimali watu wa kutosha na raslimali fedha.

“Mkaguzi wa ndani ni kioo cha taasisi yetu, Mkurugenzi bora hawezi kukosa kuzungumzia misingi ya utawala bora, ambayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa anajenga misingi thabiti ya usimamizi wa fedha za umma,” amesema bwana Nzunda.

Amesema kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa Na.9 ya mwaka 1982 pamoja na marekebisho yake, Waziri mwenye dhamana ya serikali za Mitaa amepewa wajibu wa kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa na usimamizi thabiti wa fedha.

Bwana Nzunda ameongeza kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali zimekuwa zikibainisha kuwa bado kuna tatizo kubwa la halmashauri kutotekeleza mapendekezo ya ukaguzi hasa kwa miaka ya nyuma.

“Taarifa ya CAG kwa mwaka 2016/17 ilibainisha kati ya mapendekezo 12,703 yaliyotolewa mwaka 2015/16 ni mapendekezo 4,262 sawa na asilimia 34 tu ndiyo yaliyotekelezwa kwa ukamilifu,” amesema.

Vile vile bwana Nzunda amesema kati ya maagizo 748 yaliyotolewa na kamati ya LAAC, maagizo yaliyotekelezwa na kukamilika yalikuwa 233 sawa na 31 tu.

Awali akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji wa fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Bi Miriam Mmbaga amesema kuwa kikao hicho kitafanyika kuanzia tarehe 19-26 Machi, 2019 ambapo kitawahusisha Wakurugenzi, Waweka Hazina na Wakaguzi wa Ndani kutoka Mikoa 26 na Halmashauri zote 185 nchini.

Amesema lengo la kikao hicho ni kuwawezesha Watendaji hao kujibu hoja za CAG, kuongeza uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili hoja hizo zisijitokeze tena katika halmashauri zao.

Kwa mujibu wa Bi Mmbaga takwimu za taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha 2013/14 kati ya hoja 7921 zilizoibuliwa ni hoja 2330 sawa na asilimia 29 ndizo zilizopatiwa majibu.

Kufuatia kuibuliwa kwa hoja hizo za CAG, Ofisi ya Rais TAMISEMI baada ya kupokea maagizo ya Waziri Mkuu iliwataka Wakuu wa Mikoa wasimamie na kujadili utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na kuchukua hatua ambapo jumla ya watumishi 203 kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa walichukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria.

Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa bwana Mwanyika Semroki amesema kuwa ni vyema watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanazingatia udhibiti na usimamizi imara wa fedha za umma hasa kwa kutambua maeneo au miradi iliyo kwenye hatari ya kufanyiwa ubadhilifu.




Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.