• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI Awapa Kongole Masasi kwa Kituo cha Afya

Imewekwa tar.: June 7th, 2018

“Wahenga walisema kilio kina  mwenyewe, mlilia, tukasikia, na kutokana na kilio chenu tukaja tulie pamoja na hatimaye zikaletwa fedha  shilingi milioni 400 kwa ajili ya  upanuzi wa kituo cha afya cha Nagaga na majengo yanaonekana, nawapongeza”   alieleza  Naibu Katibu Mkuu  OR- TAMISEMI  Dr. Zainabu Chaula wakati alipotembelea utekelezaji wa mradi wa  upanuzi wa kituo cha afya Nagaga unaolenga kukifanya kituo hicho kutoa huduma bora kwa wananchi wa  Kata ya Namalenga na vijiji jirani.

Dr. Chaula amesema, utekelezaji wa mradi huo umezingatia thamani ya fedha iliyotolewa kwani  majengo ni mazuri na yana ubora unaotakiwa hivyo adhima ya serikali ya kuboresha miundombinu na huduma za jamii kwa ujumla inatekelezeka kwa vitendo baada ya kuona majengo ambayo yamejengwa katika kituo hicho cha Nagaga.

Pia Dr. Chaula amewapongeza wananchi  wa Nagaga kwa ushirikiano wanaoutoa katika utekelezaji wa mradi huo na hivyo inaashiria wananchi kuwa wanatambua mipango ya serikali na kuiunga mkono kwani suala la maendeleo linahitaji ushirikiano kati ya serikali, wadau wa maendeleo na wananchi wenyewe na sio kuiachia serikali pekee.

Katika mradi huo jumla ya majengo matano ikiwemo jengo la maabara, upasuaji, wodi ya wazazi,  jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi kwa gharama ya shilingi milioni 400.

Aidha Dr Chaula amewaeleza wananchi kuwa, majengo hayo yamejengwa na mafundi wa kawaida kwa kushirikiana na wataalamu hivyo nawakumbusha vijana wenye ujuzi kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fursa za kupata  mikopo, kandarasi za ujenzi wa miradi na  huduma mbalimbali  kwani serikali imedhamiria kuwainua vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali za kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na kuwaongezea kipato.

Akizungumzia kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Nagaga  ndugu Afati Mangochi alisema kuwa wananchi wanaipongeza serikali kwa kuleta fedha za kupanua kitu hiki cha afya ambacho kikikamilika kitasaidia utoaji wa huduma za uhakika kwa  wananchi wa Nagaga na walio nje ya nagaga wapatao 129,609 sawa na 47% ya wakazi wote wa masasi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Namalenga mhe. Arafath Ismail Hassani ameahidi kuendelea kusimamia miradi huo mpaka utakapokamilika pamoja na kuhamamsisha wananchi kujitolea kwa hali na mali kuunga mkono serikali katika kuboresha na kusogeza huduma za jamii kwa wananci ikiwemo usimamizi wa miradi inayotumia fedha za serikali na wadau wa maendeleo.

Halmashauri ya wilaya ya Masasi ina jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya  47 ambapo kati ya hivyo vituo vya afya ni 2, na zahanati 31 zinazomilikiwa na serikali vingine 14 vinamilikiwa na wadau wenngine kama dini na watu binafsi.

Nyumba ya mtumishi  kituo cha Afya Nagaga

Chanzo http://www.masasidc.go.tz

 

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.