Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Msicheleweshe Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo – Dkt. Festo Dugange

Imewekwa tar.: December 6th, 2022

Na Fred Kibano – Chamwino, Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange ameonesha kutoridhishwa na ujenzi wa zahanati ya Manchali B iliyopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Dkt. Dugange amefanya ziara hiyo mapema leo tarehe 06.12.2022 katika Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma katika kijiji cha Manchali B huku akiwasisitiza Watendaji hao kuwa na utaratibu wa kujifanyia tathmini ya utendaji kazi kwani ni muda mrefu wamekaa na fedha za kuendeleza ujenzi bila sababu za msingi.

"hii ni changamoto kubwa kama tunaweza kukaa na milioni 50 ya zahanati kwa zaidi ya miezi 12 bila kukamilisha, nafikiri tunahitaji kujitathmini na kuchukua hatua, wananchi wanasubiri, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha sisi kazi yetu ni kutekeleza na kuhakikisha miradi imekamilika na wananchi wanaanza kupata huduma" amesema Dkt. Dugange.

Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt. Semistatus Mashimba kumweleza wamejipangaje ili itakapofika Desemba 12, 2022 zahanati 4 zilizopatiwa fedha ziwe zimekamilika ili ziweze kuanza kutoa huduma ya Afya kama inavyotarajiwa ambapo Mkurugenzi huyo alisema maelekezo yote wameyapokea na kwamba watayafanyia kazi ili zahanati hizo zianze kutoa huduma kwa wananchi.

Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Best Magoma amesema 2021/22022 mkoa ulipatiwa shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya uendelezaji zahanati katika mkoa wa Dodoma na matarajio ifikapo tarehe 30 Desemba miradi yote iwe imekamilika lakini pia katika mwaka 2022/2023 mkoa umepata shilingi  milioni 550 kwa ajili ya zahanati 11 na Halmashauri ya Chamwino wamepatiwa zahanati mbili zitakazokamilishwa.

Naye Peter Athman Afisa Afya akisoma taarifa ya zahanati ya kijiji cha Manchali B ambayo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 93.5 amesema ujenzi wa jengo hili unahusisha nguvu za wananchi 3,522,000 ikihusisha ukusanyaji wa mawe, mchanga na kokoto, mapato ya ndani ya Halmashauri shilingi milioni 10 na shilingi milioni 50 fedha kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kumalizia jengo la zahanati lakini kwa sasa zahanati inakabiliwa na changamoto ya nyumba ya mtumishi.

Kwa upande wake Mheshimiwa Nelson Mtundu Diwani kata ya Manchali ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa zahanati lakini ameiomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya ili kusogeza huduma kwani Kata yake inavyo vijiji vitano ambavyo havina kituo cha afya.  



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 2 May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.