Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mradi wa Fursa na Vikwazo Iliyoboreshwa Kuingizwa kwenye Majukumu ya OR - TAMISEMI

Imewekwa tar.: February 23rd, 2021

Na. Fred Kibano

Serikali imeagiza kuingizwa kwenye majukumu yake kazi zote za mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O & OD) Iliyoboreshwa ili kuhakikisha muendelezo wake unakuwa wenye tija na kuleta maendeleo miongoni mwa jamii ya Watanzania.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Bwana John Cheyo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa kazi wa pamoja kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambapo alimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga.

Amewaagiza Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Mhina na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Mpamila Madale kuandaa mipango madhubuti ya mradi huo ambayo itasaidia kuwafikia watumishi wote wa Wizara, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  ili kuimarisha utekelezaji wa mradi huo.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaagiza Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mkuu wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) kuandaa mipango na miongozo itakayowezesha kuwafikia watumishi wote wa Serikali ili kuimarisha utekelezaji wa Mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) huku muendelezo wake ukiwekwa kwenye majukumu ya kila siku ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa”

Amewataka wajumbe kujadili kwa kina mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O & OD Project) mwaka 2015 mpaka unafikia ukomo mwezi Machi, 2021 pamoja na uendelevu wake.

Amesema anajivunia timu nzima ya mradi wa O&OD kwa jitihada zao kwa kufikisha njia na malengo ya mradi kwa ajili ya utoaji bora wa huduma kwa maendeleo ya jamii.

Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kuhakikisha walau wanamwacha mtaalamu mshauri mmoja ili kuimarisha muendelezo wa mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo lakini pia kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (JICA).

Kwa upande wake Bwana Naofumi Yamamura Mwakilishi Mkazi wa JICA ofisi ya TANZANIA ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kukamilisha Miongozo ambayo imewasilishwa kupitia vikao kazi kwa Watendaji na Viongozi wa Mikoa 26 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 na kwamba itasaidia kuendeleza Mfumo wa Fursa na Vikwazo Ulioboreshwa.

Vilevile, Yamamura amesema sehemu ya uendelezaji wa mradi huo itakuwa ni pamoja na Mipango, Bajeti na Tathmini ambayo itainua uwezo wa jamii kushiriki, kuwapa nguvu, kutambua jitihada zao ikiwa ni pamoja na mahusiano baina ya jamii na Serikali.

Mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo Ulioboreshwa umetekelezwa kwenye Mikoa mitano ya Pwani (Bagamoyo, Chalinze na Kisarawe), Morogoro (Halmashauri ya Mji Ifakara, Ulanga, Mlimba na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro), Dodoma (Kondoa), Kilimanjaro (Siha, Hai na Same) na Singida (Ikungi, Manyoni, Itigi, Mkalama, Iramba, Singida Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Singida) ambapo lengo lake kuu ni kuijengea uwezo jamii kushiriki shughuli za kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao na kwenye sekta mbalimbali kama vile kujenga shule, maghala, ofisi za vijiji, barabara, kilimo na nyinginezo.  

Mkutano huo umewahusisha Wajumbe wa Uratibu wa Mradi wa Fursa na Vikwazo O&OD Ulioboreshwa. Ambao ni Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wawakilishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu. Wengine ni Makatibu Tawala wa Mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Singida, Pwani na Morogoro, Wakurugenzi wa Halmashauri 18 tajwa hapo juu, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Wawakilishi kutoka JICA waliopo nchini na wale waliopo Tokyo, Japan.


















Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.