• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Kituo cha afya Makole chapongezwa kwa kutoa huduma bora za tiba kwa wananchi

Imewekwa tar.: June 5th, 2019

Na Mathew Kwembe, Dodoma

Serikali imekipongeza Kituo cha Afya cha Makole kilichopo katika jiji la Dodoma kwa jitihada zake za kuboresha huduma za tiba, na kupelekea ongezeko kubwa la wateja kutoka  25,480 waliokuwa wakipata huduma kituoni hapo miezi mitatu iliyopita  hadi 35, 486  kufikia mwezi aprili mwaka huu sawa na ongezeko la wateja wapya 10,926 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 30.

Sambamba na ongezeko hilo, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita idadi ya wateja waliokuja kupata matibabu katika kituo hicho wanaotumia bima ya afya (NHIF) imeongezeka kutoka wateja 470 hadi 973 ambao ni karibu maradufu ya wateja waliokuwa wakipata matibabu katika kituo hicho.

Akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha Afya Makole, wakati wa ziara yake ya pili kukitembelea kituo hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Dorothy Gwajima ameelezea furaha yake kufuatia kupokea taarifa ya kituo hicho na Mganga Mfawidhi Dkt George Matiko, ambayo imeonyesha kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya utoaji huduma kituoni hapo.

Dkt Gwajima amesema kuwa ikiwa ni miezi mitatu tangu alipofanya ziara yake kwa mara ya kwanza katika kituo hicho, mnamo februari 17, mwaka huu, safari hii amefurahi kuona namna watendaji wa kituo hicho wakiongozwa na mlezi wa kituo hicho Bi Mary Shadrack walivyojidhatiti kutoa huduma bora za tiba kwa wananchi.

Amesema kitendo cha watumishi wa Kituo cha afya Makole kubadilika na kutoa huduma bora kwa wananchi kinapaswa kuigwa na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

“Nilipotembelea kituo hiki tarehe 17 februari, 2019, nilikuta kituo chenu kikiwa na malalamiko mengi ya wagonjwa hasa kero ya foleni na malalamiko ya kutoa huduma mbovu kwa wagonjwa, lakini sasa mmebadilika hongereni sana,” amesema Dkt Gwajima na kuongeza:

“Napenda kuwasihi muendelee na ari hiyo ya kutoa huduma kwani wananchi wengi wangependa kupata huduma katika vituo vya afya vya umma lakini wanakatishwa tama na huduma ma mazingira mabovu wanayoyakuta.”

Kufuatia mafanikio hayo ambayo yamepatikana katika kipindi kifupi, Dkt Gwajima ametaka vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini viige mfano wa kituo cha afya Makole.

Wakati huo huo Dkt Gwajima amewapongeza Makatibu Tawala wa mikoa ya Morogoro na Ruvuma kwa kufanyia kazi taarifa za ziara zake katika mikoa hiyo na matokeo yake viongozi hao kuamua kufanya  mabadiliko kwa timu za usimamizi huduma za afya za mikoa yao jambo ambalo litaleta mabadiliko yatakayosaidia kuongeza kasi ya usimamizi kwa watendaji wapya watakaoteuliwa badala ya ule wa mazoea kama ulivyojidhihirisha kwa wajumbe walioondolewa.

Amesema katika mkoa wa Morogoro, katibu Tawala wa mkoa huo amelazimika kuwapumzisha wajumbe 9 wa Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya Mkoa huo majukumu yao ya uongozi wa afya ili wakaendelee na majukumu ya kitaaluma katika vituo walivyopangiwa.

Wajumbe walioondolewa ni Dkt. Frank Jacob (Mganga Mkuu wa Mkoa) (RMO), Santiel Kinyongo (Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto) (RRCHCO), Salanga Maftah (Mratibu wa Huduma za Maabara) (RLT), na Florence Saka (Mratibu wa Malaria) (RMIFP)

Wengine ni Dkt. Emanuel Tenga (Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukimwi) (RTB/HIV), Leticia Nchia (Mratibu wa Huduma za Ukimwi) (RACC), Dkt. Samson Tarimo (Mratibu wa Afya ya Kinywa na Meno) (RDO), Grace Masawe (Muuguzi Mkuu wa Mkoa) na Dkt. Secondry Njau (Mratibu wa Afya ya Macho) (REC).

Aidha, Wajumbe wengine 6 wa Timu ya Afya Mkoa wa Morogoro wamepewa onyo la kuboresha utendaji wao vinginevyo nao watatolewa kwenye nafasi za uongozi mara moja.

“Ukipewa nafasi ya uongozi wa afya ngazi ya mkoa na halmashauri usimamie, ufuatilie na uchukue hatua au utoke kwenye nafsi hiyo na siyo vinginevyo,” amesema Dkt Gwajima.

Pia Dkt Gwajima amesema Timu ya Usimamizi Huduma za Afya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma pia, wajumbe wake wote wa kudumu wameondolewa kwenye nafasi zao za uongozi kutokana na uwajibikaji wa mazoea.

Katika ziara hiyo, Dkt Gwajima aliongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt James Kiologwe na Mjumbe wa timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya mkoa wa Dodoma Bi Mary Shadrack ambaye alipewa jukumu la kulea kituo hicho kwenye kipindi hiki cha maboresho.



Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.