Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

Imewekwa tar.: December 4th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo (Mb) ameonyesha kukerwa  na kasi ndogo ya  ujenzi wa barabara kutoka Martin- luther  hadi Swaswa  unaofanywa na  Mkandarasi SIKOL building Contractors Company katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo  amesema Mkandarasi huyo hana uwezo wa  kujenga  kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa barabara hiyo ambapo alianza  tangu  February, 2019 nakutakiwa kukamilika August, 2019 lakini mpaka sasa bado kazi hiyo haijakamilika licha ya kuongezewa mwezi mmoja kukamilisha hadi kufikia Desemba 30,  2019.

“Dodoma tumejenga barabara nyingi lakini hakuna ubabaishaji kama ujenzi wa Barabara ya Martin- luther hadi Swaswa, hivyo Mkandarasi huyu   uwezo wake ni mdogo na hivyo hataweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati,” amesisitiza Mhe. Jafo

Ameuagiza uongozi wa  Mkoa wa Dodoma kuhakikisha hawatoi  zabuni kwa Mkandarasi  SIKOL building Contractors Company  kwa kuwa ameonyesha kiwango kidogo cha utekelezaji wa miradi aliyopewaya  ya ujenzi wa barabara ya Martin Luther  hadi Swaswa .

“Niwaagize uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha kapuni hii haipewi tena zabuni katika Mkoa wa Dodoma kutokana na kiwango kidogo walichokionyesha katika ujenzi wa Barabara hiyo, “amesisitiza Mhe Jafo

Amesema kuwa haiwezekani Serikali ikatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara lakini baadhi ya wakandarasi wanakwamisha kwa kutomaliza kwa wakati hili jambo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kukwamisha juhudi za Serikali za kuleta maendeleo kwa jamii.

Mhe. Jafo amewaagiza wakandarasi wote nchini wanaotekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuacha ubabaishaji, bali wakamilishe miradi kwa wakati walipangiwa ili kuleta maendeleo kwa jamii

“Wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa zingatieni muda uliowekwa katika kukamilisha miradi ili kuweza kuhakikisha lengo la Serikali la kutoa huduma kwa jamii linafanyika kwa wakati,” amesema Mhe. Jafo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dr Binilith Mahenge ameitaka  bodi ya Usajili ya  Wahandisi Nchini kuhakikisha wanafanya uchambuzi  wa kina  kwa wakandarasi wenye makampuni makubwa ili kujua uwezo wao wa kufanyakazi zinazotolewa na Serikali.

Hatahivyo, Meneja wa Tarura Jiji la Dodoma Mhandisi Geofrey Mkinga amesema ujenzi wa barabara hiyo unagharimu shilingi  Bilioni 1.37 na tayari mkandarasi amekamilisha kazi kwa silimia 83  na amekatwa shilingi milioni 82 kwa ajili ya kuchelewesha kukamilisha mradi kwa wakati.

Aidha, katika ziara hiyo Mhe Jafo ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Martin-Luther hadi Swaswa, Ujenzi wa eneo la kuegesha magari makubwa (Lorry Park), Ujenzi wa Madarasa na Baabara katika shule ya Sekondari ya Itega na Lukundo.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI





Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.