• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jafo akabidhi Bil 1.7 Ruzuku kwa Vijana toka USAID

Imewekwa tar.: May 29th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) amekabidhi hundi za mfano zenye thamani ya Tsh 1,731,038,850 kwa Taasisi tisa za vijana wa Mikoa ya Mbeya, Iringa pamoja na Zanzibar kwenye hafla ya iliyofanyika kwenye viwanja vya Sido Jijini Mbeya.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Jafo amesema Ruzuku hiyo inayotolewa kwa mara ya pili sasa  itawezesha vijana kupewa ujuzi utakaowasiaidia katika kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye maendeleo  ya Taifa kwa ujumla.

“Fedha hizi zinztolewa kama Ruzuku kupitia kwa Taasisi Tisa ambazo zitafanya kazi mbalimbali ili kuwafikia vijana wa maeneo yote ambao mradi wa Inua Vijna unatekelezwa hivyo tunataka tuone mabadiliko kwa vijana wetu, tunataka tuone maendeleo ya moja kwa moja kupitia fedha hizi.

Ni vyema sasa Mradi wa Inua Vijana mkafanya tathmini ya kina kuona ni namna gani fedha hizi zinaleta mabadiliko yenye Tija kwa vijana wetu, uchumi wao umeimarika kwa kiasi gani na kama kuna sehemu ambayo bado inahitaji ufadhili nguvu zielekezwe zaidi kwenye eneo husika ili matokeo ya haraka yaweze kupatikana” Alisema Jafo.

Vijana wa sasa wanatakiwa kujengewa mawazo mapana zaidi, kupewa ujuzi utakaowezesha kuwa wabunifu na kufanya shughuli ambazo zitawaingizia kipato kikubwa cha kuwafanya kutoka kwenye kipato cha chini na kuwa watu wenye kipato cha kati Aliongeza Jafo.

“Mradi huu ni muhimu sana kwa mendeleo ya Taifa letu kwani unalenga kukuza uchumi, kupunguza umasikini na kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi kwa kuhakikisha kuwa sekta zinazogusa maisha ya watu wengi na maskini zinakuwa kwa kasi” Alsiema Jafo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye mwejeji wa hafla hii Mhe. Albert Chalamila alisema ni katika Mkoa wa Mbeya mradi wa Inua Vijana umefanikwa kubadilisha maisha ya vijana wengi ambao wamejengwa uwezo katika maeneo ya ujasiriamali, uongozi afya ya uzazi pamoja na kupewa ujuzi katika kazi mbalimbali za kuwaingizia kipato.

“Ukishindwa kumshukuru binadamu mwenzio hata Mungu sio rahisi kumshkuru mimi napenda niwashkuru sana USAID kupitia mradi wa Inua Vijana kwa kazi kubwa waliofanya katika Mkoa wangu wa Mbeya tunatambua mchango wenu na pia niombe mzidi kuwafikia vijana wengine kwenye Wilaya ambazo mradi huu haujafika ili nao wanufaike na matunda haya” Alisema Chalamila.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Happy ambaye Mkoa wake ni wanufaika wa mradi wa Inua Vijana alisema kuwa ukiwawezesha vijana umewezesha Taifa kwa kuwa vijana ndio Nguvu kazi ya Taifa nafurahia kuona mafanikio ya mradi huu kwenye Mkoa wangu na mi ntazidiki kutoa ushirikiano kila itakapohitajika ili vijana wa Kitanzania wazidi kupata hii fursa.

Aidha Mhe. Happy alisema, Miradi hii ya vijana ili iwe na Tija lazima iwe endelevu ni bora pale mradi unapoisha zile rasilimali za mradi zitakakabidhiwa kwa vijana ili waendelee kuzitumia katika kuendeleza miradi hii ambayo imeanzishwa.

Mkurugenzi wa  Mkaazi wa USAID Tanzania Andy Karas alisema zoezi la kukabidhi ruzuku kwa ajili ya vijana linafanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza zaidi ya shilingi Bil 1 zilitolewa lengo ikiwa ni kuwaunganisha vijana na fursa mbalimbali za ujasiriamali na ajira kwa kuzingatia mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo na mifugo.

Naye Mtaalam wa Vijana kutoka USAID Joyce Mndambi amesema kuwa mradi huu una nia ya kubadilisha mtazamo na matarajio ya vijana kwa kuwaendeleza katika fani mbalimbali zikiwemo ujasiriamali, uongozi na kuimarisha Afya zao.

Oscar Kapande ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Baba Watoto inayofanya shughuli zake Wilayani  Kilolo Mkoani Iringa na pia Taasisi hiyo  imepata Tsh Mil 205 kwa ajili ya kazi za vijana amesema amekwishawafikia vijana zaidi ya 100 na kati ya hao 61 ni wasichana na anawajengea uwezo  wa kujiamini  na kuweza kufanya maamuzi.

Mradi huu wa Inua Vijana ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2022. Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Zanzibar na unalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-35.


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.