Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

HALMASHAURI TAMBUENI JUKUMU LA KUSAFISHA BARABARA NA MITARO - MHANDISI MATIVILA

Imewekwa tar.: July 24th, 2024

Na OR TAMISEMI, Kibakwe, Mpwapwa

Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutambua kuwa jukumu la kusafisha  barabara na mitaro ni la kwao na si la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) huku wananchi wakihimizwa kuzitunza barabara zinazojengwa katika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI  anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa barabara na madaraja zilizojengwa kwenye kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.

Mhandisi Matavila alisema kwamba Halmashauri zielewe kwamba suala la kusafisha barabara zilizojengwa kwenye Halmashauri, Miji na Majiji yao ni jambo la kwao na hivyo wanatakiwa kuhamasishana  waweze kusafisha.

“Tumeshaletewa barabara nzuri tuzitunze ili zitusaidie sisi wenyewe, mwananchi una nyumba hapo pembeni ya barabara ni vyema kujitoa kusafisha hizo nyasi kandokando ya barabara”, alisisitiza

Kwa upande wa ujenzi wa barabara zinazotekelezwa na TARURA  wilayani Mpwapwa alisema Mji umeanza kupendeza kwani tayari ujenzi wa barabara, madaraja pamoja na uwekaji wa taa unaendelea.

Katika  Kata ya Kibakwe TARURA imeshajenga barabara ya  lami yenye urefu wa Km. 1.8 na barabara ya Km. 1 iko kwenye hatua za ujenzi ambapo lengo ni kufikia Km. 2.8 Za ujenzi wa barabara katika mji huo ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

“Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutafuta fedha za ujenzi wa barabara nchini”.

“Serikali imeona umuhimu wa maendeleo ya  barabara za mijini pamoja na kuondoa vikwazo kwa sababu yakukosekana kwa vivuko au madaraja, Mhe. Rais ametafuta fedha kwa lengo la kuhakikisha Makao Makuu ya Wilaya zote pamoja na Miji mikubwa inayokuwa angalau ziwe na lami ili kuunganisha barabara za mijini ambapo sehemu nyingi sana tayari zimejengwa barabara za lami”, aliongeza

Naye, Afisa Mtendaji wa kata ya Kibakwe Bw. Baraka Zebedayo alisema kupitia Serikali wanafanya uhamasishaji kwa wananchi kuendelea kutunza barabara kwa kufanya usafi kwenye mitaro na pembezoni mwa barabara  pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu kwenye barabara  na kila jumamosi ya mwisho wa mwezi wanafanya usafi.

Wakati huo huo Diwani wa kata ya Kibakwe Mhe. Athanas Chisanza alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa barabara na hivyo kuchochea kasi ya maendeleo katika  Kata yao na wananchi kwa ujumla.

Alisema baada ya kuwekewa lami wananchi wao wamepata maendeleo makubwa kiuchumi kwani kata yao ni wazalishaji wakubwa wa mazao hivyo imewarahisishia shughuli za usafirishaji ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo barabara hizo zilikuwa mbaya sana.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.