Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

HAKIKISHENI UANDIKISHAJI WA WATOTO WENYE UMRI WA KUANZA ELIMU YA AWALI NA DARASA LA KWANZA UNAKAMILIKA KWA WAKATI

Imewekwa tar.: January 21st, 2025

Na. OR - TAMSIEMI, Muleba Kagera

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia elimu ya Msingi Bi. Susan Nussu amewataka Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu kote nchini, kila mmoja ahakikishe uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa kuanza Elimu ya Awali na Darasa la Kwanza unafanyika na kukamilika mapema ili kuwapa fursa walimu kuendelea kufundisha.

Bi. Nussu amesema hayo leo tarehe 20/1/2025 kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bw. Adolf Nduguru wakati akifunga Mafunzo ya Walimu wa Elimu ya Awali Na Walimu Wakuu katika Chuo cha Ualimu Katoke, Kagera.

Amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 inasisitiza utoaji wa elimu bora, kuanzia Elimu ya Awali ambayo ndiyo msingi wa kwanza katika mfumo wa Elimu rasmi kote ulimwenguni. Pia amesema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Elimu ya Awali ina mchango mkubwa katika makuzi na malezi ya mtoto kiakili, kimwili na kijamii.

‘Programu ya BOOST inayotekelezwa na WyEST kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI imelenga katika kuwekeza kwa watoto wa Elimu ya Awali kwa kuandaa Kitita cha Ubora cha Kujifunza katika Elimu ya Awali ili kuimarisha ujifunzaji wa watoto wa Elimu ya Awali kulingana na hatua za makuzi” amesema Nussu

Aidha, amesema, Serikali imeendelea kutekeleza mpango wa elimu bila ada kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Sita kwa kuongeza fedha za kugharamia mpango huo kutoka shilingi bilioni 249.7 mwaka 2020/21 hadi shilingi bilioni  484.3 mwaka 2024. Jumla ya shilingi trilioni 1.304 zimetolewa kati ya mwaka 2020/21 hadi Desemba 2024. 

"Idadi ya wanafunzi wanaonufaika imeongezeka kutoka 13,888,694 mwaka 2020/21 hadi 15,298,054 mwaka 2024" 

 Ameongezea  kwa kutoa wito kwa wazazi wote wenye wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari wahimizwe kuwapeleka shule wanafunzi hao mepama iwezekanavyo ili kuepuka kukosa mafunzo kabilishi (orientation course) yanayotolewa kama msingi wa ujifunzaji katika ngazi hiyo ya elimu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndugu. Isaya Mbenja amesema anaenda kusimamia utekelezaji wa mafunzo yote yaliyotolewa kwa walimu hao kwa vitendo kwa kuzingatia mahitaji maalumu ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini.

Mafunzo hayo yalitolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu yamenufaisha walimu katika halmashauri zote 184  kwa kufundishwa mada mbalimbali zikiwemo nyenzo za kufundishia  jumla ya walimu  3,000 wa elimu ya awali ambapo jumla ya washiriki 18,564 wamejengewe uwezo wakiwemo walimu wa elimu ya awali 9670, wakuu wa shule 9,302 kutoka shule 9,302, maafisa elimu wa mikoa 26, wakuu wa divisheni ya elimu msingi 184.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.