Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Gwajima ataka Huduma Tembezi za Afya kuwa Jukumu la Pamoja

Imewekwa tar.: June 22nd, 2019

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wadau wote wanaotoa huduma Tembezi za Afya kuunganisha nguvu kwa pamoja ili huduma hiyo iweze kufikishwa katika Halmashauri zote Nchini.

Dkt.Gwajima ameyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa Afya kuwasilisha Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi kilichofanyika katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Gwajima amesema huduma Tembezi za Afya ni muhimu kufikishwa katika Ngazi ya Jamii ili wananchi waweze kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa tena kwa gharama nafuu.

“Huduma hizi zimekuwa zikitolewa na Taasisi tofauti kwa nyakati tofauti na kila Taasisi analenga eneo Fulani ambalo anachagua hivyo kuna maeneo ambayo yamekuwa yakinufaika na huduma hizi mara kwa mara lakini kuna sehemu nyingine hazifikiwi  kabisa sasa ni umefika wakati wa kukaa pamoja na kuunganisha nguvu ya wadau wote pamoja na Serikali na kupelekwa huduma hii katika Halmashauri zote ili kila mwananchi mwenye uhitaji anufaike nayo”

Kupitia Kikao hiki cha leo tutaunda Kamati ya Uendeshaji ambayo itahusisha Wataalamu wa OR-TAMISEMI, Wizara ya Afya, Asassi zisizo za Kiserikali pamoja na wadau wanaotekeleza Afua za Afya ambao watakuja na hadidu za rejea zitakazotuongoza katika kutekeleza azima yetu hii kwa ufanisi aliongeza Dkt.Gwajima.

Pia Dkt. Gwajima alisema kuwa “Tunajua tuna vituo vya kutolea huduma vya lakini si wakati wote vituo hivyo vinakuwa na madaktari Bingwa na kwa mwananchi wa kawaidia kusafiri mpaka kukutana na madaktari bingwa ni gharama hivyo tukisogeza huduma hizi tutawatibu wananchi wetu hata yale magonjwa ambayo walikuwa wameyakatia tamaa”Alisema Gwajima.

Dkt. Gwajima aliongeza kuwa Huduma hizi Tembezi zina faida zake kwanza gharama za kuwekeza katika huduma hii ni ndogo lakini inawafikia watu wengi tena kwa muda mfupi. Unafuu huu wa gharama sio kwa sisi kama watoa huduma lakini pia kwa wagonjwa ambao ndio wanufaika wa huduma hii yaani ugonjwa ambao angeweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja anaweza kupata huduma hiyo hiyo kupitia Kliniki Tembezi kwa elfu thelathini tu.

“Huduma tembezi ni msaada kwa wanyonge, wananchi wanaugua magonjwa makubwa ambayo hata akisafiri kumfuata Daktari Bingwa anaweza akafia njiani kabla hata hajakutana na huyo Daktari, kupitia huduma hii watakutanishwa na Madaktari bingwa kwa urahisi na nafuu zaidi na hapo tutakuwa tumegusa maisha ya watanzania na kuwaongezea siku za kuishi maana wangeweza kufa kwa kukosa huduma za Afya stahiki kwa magonjwa yanayowasumbua” Alisema Gwajima.

Tusipowafuata na kuwatibu wananchi wataendelea kunywa miti shamba na kwenda kwa waganga na hata wakati mwingine kupoteza maisha yao kwa kukosa matibabu stahiki hebu tuwafikie wote kupitia huduma hii ya Kliniki Tembezi alimalizia Gwajima.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula amesema agenda kuu katika Sekta la Afya ni Huduma ya Afya kwa Wote na hakuna mtu atakayeachwa nyuma hivyo ni lazima tuifikishe huduma hii ya Kliniki Tembezi kwa wananchi wote.

“Tunapoelekea katika Uchumi wa Kati ni wajibu wetu kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Afya Njema ili aweze kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato sasa hii kazi kwetu itakua rahisi tukiunganisha nguvu na rasilimali katika kutoa huduma hii ya Afya Tembezi tushirikiane kikamilifu kuleta tabasamu kwa watanzania” Alisema Dkt. Chaula.

Akiwasilisha Taarifa ya Huduma za Afya Tembezi Mratibu wa Huduma hiyo Dkt. Mombeki Domisian amesema tangu walipoanza kutoa huduma hii katika Mkoa wa Singida imeokoa maisha ya watanzania, imetoa elimu ya Kinga, imepeleka utaalamu na zaidi imetoa ushauri kwa wagonjwa kulingana na ugonjwa husika.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.