Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

DKT. MSONDE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHULE YA MSINGI KIGURUNYEMBE, AINGIA MOJA KWA MOJA DARASANI

Imewekwa tar.: April 24th, 2023

Na Mwandishi Wetu – Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Searikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde, amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Kigurunyembe iliyopo katika Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro ambapo alikwenda moja kwa moja darasani kujionea umahiri wa wanafunzi katika masomo wanayofundishwa.

Naibu Katibu Mkuu huyo alitembelea darasa la saba, la sita na la tatu ambapo katika madarasa hayo alitaka kuona umahiri wa wanafunzi hao katika kujieleza kwa lugha ya kiingereza.

Baada ya kuwahoji na kusikiliza namna wanafunzi hao wanavyojieleza, Dkt. Msonde alionesha kurudhishwa kiwango cha ujuzi wa wanafunzi hao huku akiwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na uzalendo huku akisema juhudi hizo zinaunga mkono jitihada za Serikali za kufanya maboresho katika sekta ya elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi na umahiri katika masomo yao. 

“Kama tunavyoona walimu wetu wanafanya kazi kubwa, kumsimamia mwanafunzi wa darasa la tatu hadi kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza namna hii siyo kazi ndogo. Na hii siyo kwa shule hii peke yake, ukienda shule yoyote ya msingi utaona namna walimu wanavyojitoa kufundisha wanafunzi. Hivyo, tunafarijika sana kuona walimu wetu wana mwitikio chanya katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu,” alisema. 

Pamoja na kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa, Dkt. Msonde amesema walimu wana jukumu la malezi kwa watoto ambapo wanatakiwa kuwafundisha tabia njema, uzalendo na nidhamu ili kujenga taifa la watu waadilifu wanaoipenda nchi yao.

Hata hivyo, ameeleza kuwa jukumu la malezi kwa watoto haliwezi kusimamiwa na mwalimu peke yake bali wazazi/walezi, viongozi wa siasa na dini na jamii kwa ujumla  wana wajibu kushirikiana na kumsaidia mwalimu  ili kusaidia watoto kukua katika maadili mema yanayozingatia utamaduni wa kitanzania. 

Katika ziara hiyo, Dkt. Msonde aliambatana na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Prof. Willy Komba, Katibu wa TSC, Mwl. Paulina Nkwama, Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) wa Mkoa wa Morogoro, Germana Mung’aho pamoja na watendaji wengine wa TSC ambao wapo mkoani Morogoro kwa ajili ya kikao kazi cha wadau kinacholenga kupata maoni kuhusu kuhuisha sheria na kanuni zote zinazosimamia utumishi wa walimu. 

Mwisho


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.