Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Gwajima atumia “Video Conference” kutoa maagizo kwa Wajumbe 234 wa Timu za Uendeshaji Huduma za Afya Mikoa (RHMT).

Imewekwa tar.: August 6th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima atumia mfumo wa uendeshaji wa vikao vya kazi kwa njia ya kielektroniki “video conferencing” kufanya mkutano na Wajumbe 234 wa Timu za Uendeshaji Huduma za Afya Mikoa, Wakurugenzi na Walezi wa Mikoa kutoka OR-TAMISEMI.

Mkutano huu ambao umefanyika kwa teknolojia hiyo ni wa mara ya kwanza na unalenga kupunguza gharama za safari kwa ajili ya vikao ambavyo, ajenda zake zinaweza kujadiliwa kwa njia ya kielektroniki na hivyo kuboresha ufanisi katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Akiongea kwa njia ya Video Conference kutokea Mkoa wa Kilimanjaro alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Dkt. Dorothy Gwajima amesema, kuanzia sasa atakuwa akitumia njia ya kielektroniki “Video Conference” kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wote wa sekta ya afya kujadili masuala yanayowahusu pia kutoa maelekezo na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu.

Dkt. Gwajima amefafanua kuwa iwapo angefanya kikao cha siku moja cha wadau  hao wa afya , posho peke yake bila gharama za safari na ukumbi kwa siku moja  ingegharimu takribani Tsh. milioni 30 na ukijumlisha na siku 2 za safari kuja Dodoma ingeweza fikia siyo chini ya Tsh. Milioni 100 au zaidi.

Anaendelea kufafanua kuwa, mfumo wa uendeshaji vikao kwa njia ya kieletroniki (video conference) utasaidia kudhibiti matumizi ya fedha nyingi zilizokuwa zikitumika katika uendeshaji wa vikao hivyo na kuwezesha kusaidia kutoa maagizo ambayo yatasaidia kufanya maboresho ya haraka na kuleta tija katika Sekta ya Afya nchini.

Amesema kuwa, kufanya vikao kwa kutumia mfumo huo kutasaidia kutatua changamoto zilizopo katika Mikoa na Halmashauri kwa kutoa ushauri wa haraka na kupokea taarifa za utekelezaji kwa ufanisi na kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na gharama za safari kwa ajili ya kufanya vikao.

Wakati huohuo Dkt. Dorothy Gwajima amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya na Timu za Uendeshaji Huduma za Afya nchini kuhakikisha wanafanya tathmini ya kina ili, kubaini changamoto wanazozisema kwa takwimu siyo kwa maneno tu ya jumla ambayo yanayoficha uhalisia wa changamoto husika.

“Kabla hatujasema upungufu wa watumishi tufanye mahesabu ya uwiano wa uwingi wa kazi kwa kila mtumishi kwa kutumia fomula ya WISN ambayo, tumefundishwa wote. Vinginevyo ukisubiri hadi Wizara ije ifanye basi hapo ni kwamba, RHMT/CHMT mtakuwa mmeshindwa kutekeleza wajibu wenu na badala yake mmegeuka chanzo cha changamoto” Amefafanua Dkt. Gwajima.

Dkt Gwajima amaesisitiza kufanya hesabu sahihi ili kuweza kuwapata baadhi ya wataalamu na kuwahamisha waende kwenye upungufu mkubwa zaidi wakati, zoezi la ajira likiendelea.

Vilevile, Dkt. Gwajima amewataka wajumbe hao kuhakikisha kabla ya kuandika changamoto ya ukosefu wa vifaa tiba, ni vyema wakahakiki maeneo yenye akiba ya vifaa ambavyo havitumiki ili vipelekwe maeneo yenye uhitaji mkubwa badala ya kila mara tunawaza kununua hivyo kusababisha baadhi ya vifaa kuharibika au kupotea.

Aidha amezitaka RHMT kumiliki taarifa wanazotuma Wizarani na kuhakikisha wanazituma kwa wakati kwa kuwa , kila mmoja atatetea taarifa aliyoituma kupitia vikao hivyo na uwajibikaji wake utawekwa wazi ambapo kwa sasa vikao hivyo vitakuwa vitafanyika kila mwezi kwa pamoja na kila wiki kutakuwa na ratiba ya mikoa kadhaa kuhudhuria vikao hivyo na kuwasilisha taarifa za maendeleo ya uwajibikaji.

Wakati huohuo Waganga Wakuu wa Mikoa wameupongeza mpango wa kuendesha vikao kwa njia ya Kielektroniki ambao umesaidia kutoa mtazamo mpya wa jinsi ya kukabiliana na changamoto  mbalimbali za Sekta ya Afya nchini.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.