Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Dorothy Gwajima Azindua Mwongozo wa Ajira za muda kada za Afya

Imewekwa tar.: September 15th, 2021

Na Atley Kuni- DODOMA

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini imekamilisha mwongozo wa kitaifa wa kuwawezesha wahitimu wa kada za afya ambao hawana ajira rasmi, waweze kuajiriwa kwa muda.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri mjini Dodoma.

Dkt. Gwajima, amesema, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wamekamilisha mwongozo wa Kitaifa wa Kujitolea (National Health Workforce Volunteerism Guideline) unaotoa utaratibu wa namna bora ya Hospitali na Vituo vya afya kutumia wahitimu wa kada ya afya ambao hawajaajiriwa ili waweze kutumika rasmi katika utoaji wa huduma za afya kwa njia ya kujitolea.

“Mwongozo huo ni mkakati mahususi wa kuboresha huduma za afya kwa kukabiliana na uhaba wa watumishi katika sekta ya Afya nchini hii hapa ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji na utoaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi” amesema Waziri Gwajima.

Waziri Gwajima, amesema, Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza Afua za Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi 2,726 wa kada za Afya kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, lengo likiwa ni kuikamilisha utoaji wa huduma za afya nchini.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amesema Mkutano huo ambao umebebwa na kaulimbiu isemayo Ustahimilivu wa Mifumo ya Afya katika Mapambano dhidi ya UVIKO-19; ‘changamoto na fursa’ unatoa ishara ni kwa namna gani wataalam wa afya wanavyoshirikiana kutekeleza majukumu yao wanapo kabiliana na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (UVIKO -19) tokea ulipoingia hapa nchini.

“Pamoja na changamoto zilizopo, mmeendelea kujitoa na kutumia weledi wenu katika kuihudumia jamii, hili ni jambo la kizalendo, hongereni sana, nichukue nafasi hii kuwaelekeza viongozi wote wa ngazi zote kushiriki kuwahamasisha wananchi kwenda kupata chanjo ya UVIKO -19 kwani chanjo hizo ni Salama, amesisitiza Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, amesema serikali kuanzia awamu ya tano na ya sita zimekuwa zikitoa kipaumbele katika huduma  za fya, ambapo katika mwaka fedha wa 2021/22, jumla ya Hospitali 28 zinakwenda kuanza ujenzi wa Hospitali za Wilaya ambazo hazikuwepo kabisa, aidha Tarafa zote 207 zitajengewa Vituo vya afya huku Tarafa 150 zikiwa tayari zimeshapelekewa fedha katika mwanzo wa mwaka kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Dkt. Dugange Amewakumbusha Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri, kusimamia ipasavyo rasilimali zote zinazofika kwenye maeneo yao huku akiwataka kutumia Mkutano huo kama sehemu ya darasa la kujifunza katika kukabiliana na Uviko-19  kwa kubadilisha uzoefu kutokana na changamoto kutofautiana.

Akitoa salaam za Wizara ya Afya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, amehimiza suala la uimarishaji wa utoaji wa huduma kwani Pamoja na kujenga miundombinu lakini saula la msingi ni uimarishaji wa utoaji huduma za afya, amesema watoa huduma lazima wawe na lugha zisizo za kumkera mtu anayepatiwa huduma.

Naye Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, yeye amewataka Waganga wakuu wa Mikoa kuwa mstari wa mbele katika suala la kuchanja, aidha Wizara itafatilia kujua Mkoa na Halmashauri kinara katika zoezi la kuchanja chanjo ya Uviko-19.

Mapema akiongea  katika Mkutano huo, Dkt. Florence Temu, kutoka AMREF na mwakilisi wa Non state Actors, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudu kubwa zinazo chukuliwa katika mapambano dhidi ya Uviko-19, na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali.

“Awali kulikuwa na vituo vya kutolea huduma za chanjo 500 lakini kwa takwimu za sasa  inaonesha idadi ya vituo hivyo imeongezeka na kufikia 1500, hii ni hatua kubwa, tunaimani Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau lakini pia kuimarisha mifumo ya utoaji wa taarifa za Uviko-19. Amesema Dkt. Florence.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.