Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mgogoro Wilaya ya Chemba Watatuliwa

Imewekwa tar.: May 7th, 2021

Na Nteghenjwa Hosseah- TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu, ametatua mgogoro wa kiutalawa uliodumu kwa muda mrefu ambao ulisababisha kuzorota kwa utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Waziri Ummy amezitaka pande mbili hasimu, watendaji na madiwani, kumaliza tofauti zao na badala yake kuwa kitu kimoja, kufanya kazi kwa mshikamano, kuheshimiana na kupendana.

Kikao hicho kilichofanyika mapema hii leo chini ya Waziri Ummy, alibaini chanzo cha mgogoro ni mgawanyiko mkubwa kati ya waheshimiwa madiwani, Menejiment ya Halmashauri pamoja na Menejimenti kutokuwa na mshikamano katika utendaji wa kazi.

Sababu nyingine ni ushirikishwaji mdogo wa madiwani kwenye baadhi ya maamuzi ya Halmashauri pamoja na kutokulipwa stahiki zao kwa kipindi kirefu sasa, kitu ambacho kimechochea kuzalisha madeni yanayo athiri Halmashauri kwenye utendajikazi.

Aidha, ukusanyaji mapato usioridhisha wa makusanyo ya ndani na matumizi yasiyo sahihi ya mashine za kukusanyia mapato (POS) pamoja na kuchelewa kupeleka makusanyo Benki na matumizi ya fedha kabla yakufikishwa benki kwanza (Fedha mbichi).

Mhe. Ummy amebaini, upelekaji mdogo wa fedha kwenye miradi ya maendeleo pamoja na kutotumika vema kwa fedha za maendeleo   katika shughuli za maendeleo na badala yake fedha zimekuwa zikitumika   kwa ajili ya posho za safari, vikao na semina.

Baada ya majadiliano ya muda takribani ni saa mbili, Mhe. Ummy, alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha, wataalam na madiwani wanafanya kazi kwa ushirikiano bila kuhasimiana miongoni mwao, kwani migogoro haijengi bali inabomoa.

Pia amezitaka Halmashauri kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na kuhakikisha asilimia 40 ya fedha zinazokusanywa zinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja kama vile shule, hospitali na masoko.

“Nazikumbushe tena halmashauri zote nchini  kuwa, fedha za maendeleo nataka ziende kwenye maendeleo, miradi ile ambayo inatatua changamoto za wananchi moja kwa moja kama madarasa, madawati, matundu ya vyoo, zahanati, vituo vya afya, sio kulipana posho za safari, vikao au semina wakati miradi ya wananchi mmeiacha imelala” alisema Ummy.

Aliwataka watendaji wote waliopewa dhamana ya kukusanya mapato ya ndani ya halmashauri kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria, uaminifu na uadilifu wanapo tekeleza jukumu hilo, huku akionya kwamba wale wote watakaokwenda kinyume wata ondolewa katika nafasi hizo.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy, amesisitiza kuongeza udhibiti wa mifumo ya kukusanyia mapato katika halmashauri (Internal Control) na kuhakikisha watumishi wote wanaokabidhiwa mashine za kukusanyia mapato  wanazihifadhi vizuri bila kutoa namba za siri na jina la mtumiaji.

Amewahimiza watumishi wote wanaokusanya mapato kuhakikisha wanawasilisha fedha za makusanyo benki ndani ya saa 24 baada ya kufanya usuluhisho na kutoa ankra ya malipo kutoka kwa mhasibu wa halmashauri.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.