• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Bilioni 35 zatumika Kujenga Miundombinu ya Shule za Msingi

Imewekwa tar.: December 12th, 2019

Serikali ilipeleka zaidi ya shilingi  bilioni 35 kwenye shule za msingi na Awali  kwa ajili ya ujenzi wa    madarasa 2,897  na vyoo 533 ili kukabiliana na changamoto ya miundombinu mashuleni hadi kufikia mwezi Juni, mwaka huu.

Dkt. George Jidamva Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Msingi OR-TAMISEMI ameyasema hayo wakati akifunga kikao  kazi cha  Elimu ya Awali chini ya Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu ‘Children in Crossfire’ kwamba lengo lilikuwa ni kukabiliana na changamoto iliyotokana na Mpango wa elimu msingi bila malipo ambao ulipelekea kuwa na idadi kubwa ya uandikishwaji  wa wanafunzi hasa kwa madarasa ya Awali na la Kwanza.

Amesema jumla ya madarasa ya awali yapatayo 16129 yamejengwa,  mafunzo ya Mtaala mpya, kutoa Miongozo ya walimu, vitabu vya kiada na hadithi kwa Elimu ya Awali yamefanyika na hivyo kutachangia kuboresha elimu ya awali nchini.

Jidamva amesema Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu umechangia kuinua ubora wa Elimu ya Awali kwenye shule za msingi kwa kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa zaidi ya wanafunzi 10000, kuwapatia mafunzo walimu wa Awali 99, kutoa mafunzo kwa wadau ngazi ya Wilaya, kuhamasisha suala la lishe shuleni ikijumuisha  maji safi na salama ya kunywa, Ushiriki wa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni na Matumizi ya vifaa vinavyotokana na mazingira halisi.

Kwa upande wake Craig Ferla ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Children in Crossfire amezishukuru wizara zote mbili Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuwapongeza washiriki wote ambao wameshiriki katika mijadala yote wakati wa kikao kazi.

Akitoa neno la shukrani, Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Agripina Kanyahubunza amelishukuru Shirika la Children in Crossfire kwa kuuchagua mkoa wa Dodoma kuwa sehemu ya mradi na kwamba utekelezaji wa mradi utaanza mara moja.

Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu unalenga kuboresha mazingira ya Elimu ya Awali na unafadhiliwa na ApexHousing Association ya Ireland ya Kaskazini kupitia shirika lake la Children in Crossfire Tanzania. Mradi unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Morogoro na kwa sasa wilaya za Chemba na Kongwa mkoani Dodoma.

                                       Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.