Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Ummy; Uuguzi ni Taaluma sio Siasa

Imewekwa tar.: May 12th, 2021

Nteghenjwa Hosseah, Manyara

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wauguzi ni miongoni mwa wataalamu wa Afya wanaopaswa kuheshimiwa na kupewa thamani inayostahili na wasichukuliwe kisiasa.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani yakiyofanyika Mkoani Manyara tarehe 12 Mei,2021.

Amesema  uuguzi ni fani adhimu na kuwataka viongozi wa Mikoa na Wilaya kuacha kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

“Viongozi wa Mikoa na Wilaya niwatake kuelewa kuwa uuguzi ni taalamu adhimu na muache kuamuru wawekwe ndani au kuwachukulia hatua kali ambazo haziendani na taalum yao kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi, hili tuliache mara moja,”amesema

Ameongeza "Kama Muuguzi amekosea akashitakiwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga ambapo atachukuliwa hatua kwa matakwa ya taaluma yake na sio kwa utashi wa kisiasa.”

Hata hivyo, amesema kiongozi yeyote atakayemuweka ndani muuguzi  awe amethibitisha ameiba lakini  kwa tuhuma nyingine akashitakiwe kwenye Baraza lao la Kitaaluma.

Pia Mhe.Ummy amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kuwakatalia wauguzi kwenda kusoma mara wanapopata fursa za kwenda kujiendeleza kielimu.

"Wauguzi lazima wathaminiwe kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wagonjwa sababu mara zote ukienda hospitali Daktari atakuona kwa muda mchache sana na wakati mwingi utakuwa na nesi katika kukuhudumia hivyo wapewe moyo,"amesema.

Amewapongeza na kuwashukuru Wauguzi kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa wimbi la ugonjwa wa Corona na amewataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuokoa maisha ya watu.

Akijibu hoja zilizowasilishwa na Wauguzi katika risala yao, Waziri Ummy amesema suala la muundo linafanyiwa  kazi na lilishawasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua zaidi.

Mhe. Ummy amesema kwa sasa  Madaktari na wauguzi wafanye  kazi kama timu moja ili kuleta matokeo chanya kwa jamii inayowategemea na hayo ya kiutawala yataendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi.

Kuhusu posho ya majukumu,  amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaangalia ni namna gani inaweka mazingira bora kwa wauguzi walioko TAMISEMI kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana.

"Ofisi yangu itahakikisha inatoa kipaumbele katika kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi wa Afya kwa kujenga nyumba za kutosha ili watumishi hao waweze kukaa kwenye vituo vyao na kufanya kazi kwa amani,"amesema.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ummy ametoa zawadi ya sh.500,000 kwa Muuguzi Aldolefina Shayo wa Zahanati ya Kilangare iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ambaye amevunja rekodi ya kuhudumia wagonjwa hamsini kwa siku bila kunung’unika na leo ameshindwa kushiriki maadhimisho hayo kwa kuwa yuko peke yake kwenye zahanati hiyo na hakuna mtu wa kumsaidia.

Waziri Ummy amesema katika ajira mpya zilizotangazwa watapelekwa wauguzi wawili na Mganga mmoja ili kuboresha zaidi huduma za Zahanati hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA.

    May 19, 2025
  • MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WAPEWA SOMO USIMAMIZI WA MIRADI NA USULUHISHI WA AKAUNTI

    May 19, 2025
  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.