Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu atoa siku 15 kukamilika kwa Hospitali ya Uhuru

Imewekwa tar.: November 20th, 2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim  Mjaliwa (Mb)  ametoa siku 15  kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  na Suma JKT  kuhakikisha  ujenzi wa Hospitali ya  Uhuru  unakamilika ifikapo disemba  5, 2020.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo leo Jijini Dodoma Mhe. Majaliwa amesema Hospitali ya Uhuru ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuimarisha  utoaji huduma  katika Sekta ya afya ambayo inaanzia kuboresha kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa na Hospitali za Magonjwa makubwa.

Anaendelea kufafanua kuwa Serikali  imekuwa mstari wa mbele  kuhakikisha inaboresha huduma za afya  kwa lengo la  kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo imejikita katika kuhakikisha miradi yote ya kimakakati  inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika

“ Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa majengo (TBA),  Suma JKT, hakikisheni ujenzi wa Hospitali hii unakamilika kwa wakati, fanyeni kazi usiku na mchana, jengeni vibanda na kuhamia  kwenye eneo la ujenzi, ongezeni wafanyakazi ili kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa” amesisitiza  Mhe. Majaliwa

Mhe. Majaliwa amesema miradi ya Kimakakati inatakiwa ikamilike kwa wakati na Watanzania wanahamu ya kuona miradi inakamilika  na kuanza kutoa huduma hivyo fanyeni kazi kwa weledi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo muhimu kwa jamii

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ujenzi wa Hospitali ya Uhuru imekadiriwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 3.995 na kiasi kilichotengwa ni shilingi bilioni 3.410 ambapo zaidi ya  shilingi milioni 995 zilikuwa ni fedha za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika  na shilingi bilioni 2.415 ni gawio la kampuni ya simu ya Airtel.

Naye Msaidizi wa Mkuu wa JKT Colonel Laurence Angelo Lupenge amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru umefikia asilimia 92 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la mradi,kuchimba na kujenga msingi, kujenga “frame” ya jengo pamoja na kuta, kupiga “plaster” kuta pamoja na” skimming”, kuweka njia za mifumo ya umeme,kupaua na kufunga gypsum board,kuchimba mashimo ya maji taka na kuweka “rough floor” kwa ajili ya kuweka vigae

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.