Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

WAZIRI BASHUNGWA ASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 5 KITETO

Imewekwa tar.: July 28th, 2022


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagiza kusimamishwa kazi na kuhojiwa na Taasisi Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) watumishi watano kutokana kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya Kiteto mkoani Manyara.

Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo wakati wa ziara yake Wilayani hapo tarehe 28.07.2022.

Watumishi hao ni  aliyekuwa Mweka Hazina Ndugu Nassoro P. Mkwanda na Mhasibu wa Mapato Ndugu Christopher G. Mwigani, Kaimu Mwanasheria wa Halmashauri Ndugu Joseph J. Hoza, Kaimu Mweka Hazina Ndugu Hadija Boffu pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Nakaji Mollel.


Kati ya hao Ndugu Nassoro Mkwanda aliyehamishiwa Mafinga Mji, Khadija Bofu aliyehamishiwa Songea Manispaa na Christopher Mwigani ambaye amestasfu wote wanatuhumia kuhamisha fedha na kuweka kwenye akaunti ya amana isiyo na vifungu vya matumuzi na wanatakiwa kurejeshwa kwenye Halmashauri hiyi kujibu tuhuma hizo.


Pia Kaimu Mkuu wa kitengo cha manunuzi Nakaji Melateki Mollel ambaye aliidhinisha Sh milioni 191.9 kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi bila kufauta taratibu sambamba na Sh milioni 235.5 alizolipa mkandarasi wa kuchimbia visima bila kuzifanyiwa tathimini na Khalfan Hinga aliyetoa kazi hiyo bila kufanyika tathimini.


Pia amekemea tabia ya kuwahamisha watumishi waliofanya vibaya kwenye halmashauri na kusisitiza kuwa atawafuata popote walipo.


Bashungwa ametoa maagizo hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake wilayani Kiteto mkoani Manyara kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) 2019/20 na ile ya mwaka 2020/21 imeelekeza watumishi hao kuchukuliwa hatua kutokana na makosa hayo.


" Nilishakataza tabia ya mtumishi anafanya madudu halmashauri A na anahamishia halmashauri B, mtu alifanya madudu na kuhamisha tutamfuata huko huko. Maelekezo ya CAG lazima yatekelezwe kwa mapana yake hawa watumishi wanatakiwa kuwa Takukuru wanachunguzwa. Hawa watumishi wafutuliwe na sheria ichukuwe mkondo wake."


" Kwenye hili hatutanii, hiyo aliyeko Mafinga na wa Songe waje wajibu tuhuma zao na huyo Hoza aliyekwenda Dodoma huko huko Sheria ifuate mkondo wake. Hii tabia ya kuhamisha hamisha mtu anatenda madhambi anakwenda kwenye halmashauri anafuatwa huko huko, sheria zipo maabusu zipo, sasa kwa nini tubembelezane?


" Nimepewa kazi ya kusimamia, subiri muone, nitakwenda kwenye kila Halmashauri na hizi taarifa haziozi ukifanya mkosa halmashauri A ukaenda B nitakufuata huko huko, haiwezi kuwa kwenye utumishi wa umma na si msafi."


Pia Bashungwa alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere kuhakikisha wanaodaiwa kiasi cha Sh milioni 224.5 ambazo zilioneshwa kukusanya lakini hazikufika Benki kuwa wamerudishwa sambamba na kupiga mnada mali za mtumishi ambaye hakupeleka fedha benki ili kufikia fedha za Serikali.


Aidha, Bashungwa alisema kuna haja ya kuhoji Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri pale panapokuwa na ubadhilifu wa fedha kwa sababu ndio wanaohusika usimamizi.


Alisema ni lazima wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia ipasavyo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa ubainisha na kuchukua hatua kwa wakati.


" Tusisubiru na kukaa nyuma mpaka CAG anakuja kutukagua na kufanya chambuzi ndio tuchukue hatua, Tunapaswa kuchukua hatua kwa wakati. Katibu Tawala wa Mkoa ndio Mtendaji Mkuu na  sheria imeampa mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu kwa mtumishi yeyote ambaye yuko kwenye Mkoa ambaye anapenda tofauti na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma."


Pia ashungwa amekema tabia ya hamashauri kushindwa kuhuisha leseni za biashara kwa muda jambo ambalo linakosesha mapato.


Taarifa ya CAG imeonesha halmashauri hiyo ilikosa mapato takribani Sh milioni 177.3 ambazo halmashauri ingezipata endapo wangehuisha leseni za biashara kwa mujibu wa taratibu.

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.