• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Wanufaika wa kwanza Elimu Msingi bila Malipo kuanza Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne

Imewekwa tar.: November 3rd, 2019

Wanafunzi  wa Awamu ya Kwanza walioanza masomo yao ya Kidato cha Kwanza kupitia mpango wa ElimuMsingi Bila Malipo iliyoanza kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wataanza Mitihani yao ya Kuhitimu Kidato cha Nne mapema Kesho Tarehe 04/11/2019.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo alipozungumza na Waandishi wa habari Kwenye Ofisi ndogo za Wizara Magogoni Jijini Dar es Salaam Tar. 03/11/2019.

Amesema Mtihani wa kuhitimu Elimu ya Sekondari, Kidato cha Nne mwaka 2019 unatarajiwa kufanyika kote nchini kuanzia tarehe 04 hadi 22 Novemba, 2019. Sambamba na mtihani huo, upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (unatarajiwa kufanyika tarehe 11 hadi 22 Novemba, 2019  na Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika tarehe 20 na 21 Novemba, 2019 kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

“Niwakumbushe Watanzania wenzangu kuwa, Wanafunzi wanaoanza Mitihani yao kesho Jumatatu ya Kuhitimu Kidato cha Nne walianza Kidato cha Kwanza Januari, 2016 mara baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia Madarakani. Kwa maana nyingine, hawa ndiyo wanafunzi wa Awamu ya Kwanza walioanza masomo yao ya Kidato cha Kwanza kupitia mpango wa ElimuMsingi Bila Malipo, sisi kama Serikali tunajivunia hilo”» Alisema Jafo

Aliongeza kuwa jumla ya Watahiniwa 485,866 (wavulana 229,838 na wasichana 256,028) wanatarajiwa kufanya Mitihani hiyo ya kuhitimu Kidato cha Nne. Kati ya hao, watahiniwa wa shule ni 433,052 na watahiniwa wa kujitegeme ni 52,814.

“Kwa mwaka huu kuna ongezeko la watanihiwa 5871 sawa na asilimia 1.37 ukilinganisha na wahutimu wa mwaka 2018 ambao walikua 427,181 ilihali mwaka huu 2019 Watahiniwa ni 433,052 “. alisema Jafo.

Alifafanua kuwa Takwimu zinaonesha Idadi ya Wanafunzi wanaohitimu Kidato cha Nne imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kuanzia 2016 wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne walikuwa 349,524, 2017 wanafunzi 317,777, 2018 wanafunzi 427,181 na mwaka 2019 wanafunzi 433,052.

Kwa sababu hiyo, kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu, jumla ya wanafunzi 83,528 sawa na asilimia 23.9 wameongezeka alisema.

Jafo aliongeza kuwa  kutokana na takwimu hizi ni dhahiri kuwa mahitaji ya fursa elimu yanaongezeka miongoni mwa jamii yetu na Watanzania waliowengi hasa wa maeneo ya Vijijini sasa wanapeleka watoto wao shule bila kushurutishwa kama ilivyokuwa hapo awali.

“Takwimu hizi pia zinatutaka sote – Serikali, Wananchi na Wadau wengine wa elimu kuungana pamoja kuhakikisha kuwa tunaisaidia Serikali katika kuchangia maendeleo ya Elimu kwa watoto wetu na kwa vizazi vyetu vijavyo “alisema Jafo.

Wakati huo huo Jafo alielezea namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuwekeza kwa Kiwango kikubwa katika elimu na kusema kwa mwaka 2019/20, Serikali imetenga bajeti ya shilingi 288,485,000,000.00 kutekeleza Mpango wa Elimu msingi bila malipo kwa wanafunzi wote kuanzia elimu ya Awali hadi Kidato cha Nne.

Pia Serikali itaendelea kutoa fedha ya chakula kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita kwa shule zote za umma alisema.

Aidha, Jafo alitumia fursa hiyo kuwataka Viongozi na Watendaji wote wanaoshiriki katika usimamizi na uendeshaji wa Mitihani hiyo kufanya kazi zao kwa weledi, maadili na kwa kufuata sheria, Kanuni na Taratibu za Usimamizi na Uendeshaji wa Mitihani hiyo kama ilivyoelekezwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Serikali isingependa kusikia changamoto zozote za makusudi zitakazosababishwa na wanaohusika na usimamizi na uendeshaji wa mitihani hiyo.

Ifahamike kuwa tangu Mpango wa ElimuMsingi Bila Malipo uanze Januari, 2016, jumla ya shilingi 937,548,685,734.72 zimetumika kugharamia elimu ya watoto wetu.

Jumla ya wanafunzi takribani milioni kumi na mbili kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Sita wanafaidika na Mpango huo.

Na. Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI




Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.