• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto

Imewekwa tar.: June 8th, 2018



Jengo la Mama na Mtoto liliojengwa katika Kituo cha afya cha Hamai, 
kilichopo katika Kata ya Songolo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.


Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi  wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya  katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.

Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya  hasa vijiji vya jirani ambavyo ni  Murongia, Itolwa , Jangalo, Jinjo, Kinkima na Kirerechangombena ambao wote hupata huduma katika kituo hicho.

Bw. Msigwa amesema mwaka 2015 wanawake wa Kata ya Songolo waliamua kijutolea kujenga jengo la Wodi ya Mama na mtoto kutokana na kuwepo kwa jengo moja la wodi ya Mama na Mtoto jambo ambalo lilikuwa likisababisha msongamano wa wamama wajawazito sababu hii ilipelekea wanawake kuamua kuchimba msingi na kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa  wodi hiyo ndipo serikali ilipoamua kujenga jengo hilo mwaka 2018.

Bw. Msigwa ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya cha Hamai ambacho kitasaidia wananchi maskini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

Amesema kituo hicho kimejengewa wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi ambapo mpaka sasa tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 291.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Charles Kiologwe ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya chemba kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo yanaonyesha uhalisia wa matumizi ya fedha zilizotumika ukilinganisha na ubora wa majengo.

Aidha ameutaka uongozi wahuo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na wanapoishi.

Naye Bi Martha Mariki Afisa afya Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameutaka uongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha maeneo ya taasisi yanapimwa na kuwa na hati miliki, pia kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti kama kipaombele cha kuweka uzio wa maeneo ya taasisi ili kuepusha  maeneo mengi kuvamiwa na wananchi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe akitoa maelekezo kwa uongozi wa 
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha 
afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, 
ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima wakati walipotembelea 
Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
 Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
 ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, 
kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma


Anaandika Angela Msimbira,  OR-TAMISEMI

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.