Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wakuu wa Mikoa watakiwa kukamilisha ahadi kupata fedha za GPE

Imewekwa tar.: August 31st, 2023

Na Fred Kibano – Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa walioahidi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 465 kama ahadi ambazo zitaisaidia nchi kupata fedha za ruzuku (grant) kiasi cha Dola milioni 50.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi iliyo chini ya Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (Global Partnership for Education) ameyasema hayo leo tarehe 31.08.2023 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kama mgeni rasmi katika hafla iliyohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa  na Wadau wa Elimu kutoka mikoa yote Tanzania Bara.

“tumeshasikia jinsi ahadi zilivyotolewa, zaidi ya shilingi Bilioni 465, matumaini yangu walioahidi watatoa, ahadi ni deni, Wakuu wa Mikoa mmetoa ahadi wenyewe hapa” amesema Mheshimiwa Jakaya Kikwete.

Aidha, Kikwete amesema miradi ya GPE nchini, ilifadhiliwa kwa awamu mbili za mwaka 2014 hadi 2018 na 2018 hadi 2023 ikihusisha ujenzi wa madarasa mapya ya shule za msingi 2,980, mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum 14, matundu ya vyoo 7,673, shule mpya 98, shule mpya 18, nyumba za walimu 94, ukarabati wa vituo vya walimu 13 (TRC), ujenzi na uendeshaji wa vituo vya walimu 12, uendeshaji wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MEWAKA) na ununuzi wa vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia kwa walimu na wanafunzi.

Kwa upande wake Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha mgeni rasmi amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga imani kubwa kwa Sekta Binafsi nchini na ndio maana Wadau wameitikia kwa kiwango kikubwa na kuendelea kutoa michango yao kwenye elimu hapa nchini na hivyo ni jambo jema kwa wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais TAMISEMI kutambua mchango wa Wadau kwenye Sekta ya Elimu nchini.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Adolf Ndunguru ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Wadau, kuanzisha ‘Kanzidata’ kwa kila mkoa ili kurahisisha ufuatiliaji na tathmini ya ahadi zilizotolewa lakini pia kuendelea kuwaelimisha Wadau kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Mpaka sasa Washirika wa GPE Duniani wanatoa msaada wa kifedha kwa nchi 88 ili kuinua Sekta ya elimu na kutimiza lengo la kutomuacha nyuma mtoto yeyote katika kupata haki ya elimu.

Katika ahadi zilizotolewa mkoa wa Mara umeibuka kidedea kwa kutoa ahadi ya Shilingi Bilioni 155 wakati Dar es Salaam ukiahidi kutoa Shilingi Bilioni 20.



Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.