• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Wakurugenzi Mamlaka za Serikali za Mitaa watiwa Mtegoni

Imewekwa tar.: January 7th, 2021

Na Atley Kuni, KAGERA

Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za mitaa nchini, wamewekwa katika sintofahamu ya nyadhifa zao pamoja na wasaidizi wao endapo watashindwa kufikia viwango vya makusanyo ya mapato vilivyo kubalika kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambacho ni asilimia 85.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Selemani Jafo akiongea kwa Nyakati tofauti wakati wa ziara yake kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa ziara ambayo inakwenda sambamba na kufanya vikao vya ndani na watumishi, ameendelea kusisitiza kwamba, wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa watapimwa pamoja na vigezo vingine lakini pia suala la ukusanyaji wa Mapato kwenye Halmashauri wanazo ziongoza.

“Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, ajenda kubwa ya Mhe. Rais imekuwa ni ukusanyaji wa mapato, hili tumeliimba kwa kipindi chote cha miaka mitano iliyopita, sasa tufike mahali tusema basi, haiwezekani leo ni Mwezi Januari 2021, nusu ya Mwaka wa Serikali wa 2020/21 imeisha lakini  wewe Mkurugenzi na wataalam wako katika Halmashauri yenu hamjafikisha hata asilimia 30 hii ni aibu” Amesema Mhe. Jafo

Mhe. Jafo, amesema, wapo baadhi ya watendaji wanaofikiri adhabu itawagusa Wakurugenzi pekee yao, amesema kuwaza hivyo sio sahihi, bali katika wakati wa sasa adhabu hiyo itakwenda sambamba na watu wote wanaoguswa na mnyororo huo wa ukusanyaji wa mapato.

“Ndugu zangu hakuna Halmashauri ambayo itaweza kujiendesha endapo itashindwa kukusanya mapato ipasavyo, hivyo kama mwaka wa jana tuliweka wastani wa asilimia 81 lakini tukafika asilimia 94, ni matumaini yangu kwa mwaka huu haitatokea Halmashauri ikakusanya chini ya asilimia 85” alisisita Waziri Jafo.

Katika hatua nyingine, Waziri jafo, amewataka watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa fitna na majungu na badala yake wajitahidi kufanya kazi kwakupendana ili waweze kuacha kumbukumbu (Legacy), pindi wanapo staafu utumishi wa umma.

“Asilimia zaidi ya 80 ya muda wenu  ninyi watumishi wa umma mnautumia, mikiwa eneo la kazi, hivyo ni rai yangu lazima muishi kwakupendana ninyi kwa ninyi, wapo baadhi ya watu, wao kila kiongozi anapofika yeye ni wa kwanza kupeleka fitna na majungu, niwaambie hiyo sio tabia nzuri, amesema Jafo.

Kuhusiana na suala la upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma, Waziri Jafo amesema suala hilo lipo chini ya Himaya ya Mkurugenzi  kwa Ushirikiano wa Karibu na jopo la Menejimenti ya Halmashauri husika.

“Ndugu zangu cheo hapandishi Mkuu wa Nchi wala mimi Waziri wa Nchi, upandishwaji wa vyeo unaanzia katika ngazi unayofanyia kazi kwakuweka katika mipango ya bajeti, lakini inashangaza unakuta mtumishi hajapanda cheo kwa miaka sita na kinachofuata ni kutoa lawama kwa uongozi wa juu, kumbe tatizo lilianza kwa mkuu wako wa idara kutokukuweka katika bajeti” amesema Jafo.

Akitoa Salaam za Mkoa huo kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Brig.Gen. Marco Gagut, amempongeza Mhe. Jafo kwa Kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na wananchi wa Jimbo hilo, lakini akampongeza zaidi kwakuaminiwa na Mhe. Rais na kurejeshwa tena katika Ofisi hiyo kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Waziri jafo akiwa mkoani Kagera, ametembelea Hospitali, Vituo vya Afya pamoja shule kisha kufanya mikutano miwili na watumishi wa umma katika Halmashauri za Wilaya za Biharamulo na Ngara, ambapo sehemu zote alizopita ameendelea kuwasisitiza watumishi kufanya kazi kwa kupendana na kuacha tabia ya majungu na fitna. Aidha katika ziara hiyo Mhe. Waziri Jafo ameridhishwa na kasi ya Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Kagera.

MWISHO.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.