• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Vikundi 20 Ukerewe vyapatiwa sh milioni 51 kujikwamua kiuchumi

Imewekwa tar.: February 15th, 2021

Na Stephen Msengi, Ukerewe.

Jumla ya mikopo yenye thamani ya Sh 51,744,000 ilitolewa kwa vikundi 20 vya wanawake, vijana na walemavu katika Halmashauri ya Ukerewe katika mwaka wa fedha 2018/2019 ili kuwawezesha wanavikundi hao kujikwamua dhidi ya lindi la umasikini.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii  wa Halmashauri hiyo Cecilia Oswago ameeleza kuwa fedha hizo zilitolewa kwa vikundi 13 vya wanawake, 4 vijana na 3 watu wenye ulemavu vikiwa na jumla ya wanufaika 307.

Amesema kuwa kiasi hicho kimetokana na asilimia 10 ya mapato halisi ya ndani ya halmashauri hiyo na kuwa mikopo hiyo imelenga kuwawezesha wananchi wa ukerewe kutoka kwenye makundi hayo kujikwamua na lindi la umasikini kwa kujishughulisha na kazi mbalimbali.

Miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni Kikundi cha Vijana Chapakazi cha Nansio Ukerewe ambacho kupitia Mwenyekiti wake Alex Kabuka, licha ya kukiri kupokea kiasi cha sh.milioni tano kwa ajili ya kununulia pikipiki mbili za kikundi chake, ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwawezesha vijana kujikwamua na lindi la umasikini..

“Tunaishukuru serikali kwa mkopo huu kwani umetuwezesha kununua bodaboda mbili za kubeba abiria, walau sasa tunahudumia familia zetu na tunaweza kuanza kurudisha mkopo,” amesema.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi Cha Ushirika Sokoni kinachojishughulisha na ushonaji nguo Imelda Chrisanti ameishukuru serikali kwa kuwapa mkopo huo wa sh.milioni nne ambao umewawezesha kupanua wigo wa biashara yao  na kuanza kuuza nafaka kama mchele na mahindi kwa kuchukua meza mbili sokoni na kuwawezesha kuuza kwa wingi na kutengeneza faida na kuanza kurejesha mkopo huo.

“Mpaka sasa tumerejesha kiasi cha Tsh 3,840,000/- hii ni kutokana na mgawanyo tuliojiwekea katika milioni 4 biashara ya Ushonaji tuliongeza milioni moja na kuanzisha biashara ya kuuza nafaka kwa milioni tatu,” amesema Chrisanti.

Naye Deusdedith Mtobesha kutoka kikundi cha walemavu cha Bukongo ameilezea mikopo hiyo kama mkombozi mkubwa kwao kwani kupitia mkopo wa sh milioni tano walioupata umewawezesha wao kuongeza wigo wa biashara yao kupata shughuli za useremala na utengenezaji wa samani na mizinga ya kufugia nyuki.

“Kikundi kimefanikiwa kuongeza biashara ambapo mbali na shughuli za Useremala na kutengeneza mizinga ya nyuki wanauza mbao kwa jamii inayowazunguka na kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari kwa kadri wateja wanavyopatikana,” amesema na kuongeza:

 “Kwa mwezi disemba mpaka sasa tumefanikiwa kutengeneza mizinga 100 na madawati 50 na kutuwezesha kurejesha kiasi cha sh. 1,250,000 kufikia sasa,’’ amesema Mtobesha.

Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inatekeleza sera ya taifa ya mwaka 2019 inayohusu utoaji wa mikopo wa asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo mgawanyo wa asilimia kwa vikundi vya wanawake ni asilimia 4, vijana ni asilimia 4 na watu wenye ulemavu ni asilimia 2.

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BARABARA YA MVUMI KUWEKWA LAMI KM 3

    May 26, 2022
  • PROF. SHEMDOE AZINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI 8 KWA KUTOKUTENGE FEDHA ZA LISHE

    May 25, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA ASIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA JIJI, MAAFISA WATANO ARUSHA

    May 24, 2022
  • WAKUU WA MIKOA SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE HALMASHAURI

    May 24, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.