Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Uwekezaji wa Elimu umguse Mwalimu – Mhe Doto Biteko

Imewekwa tar.: March 13th, 2024

Na. Fred Kibano, Dar es Salaam

Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema uwekezaji unaofanywa katika Sekta ya Elimu ni lazima umguse mwalimu kwani ndiye mwenye dhamana na masuala yaliyopo kwenye mfumo wa elimu.

Mhe. Biteko ameyasema hayo mapema leo Machi 13, 2024 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuzindua Programu ya Kuboresha Kada ya Ualimu inayolenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

“mwalimu ndiye rasilimali kuu inayofanya rasilimali nyingine ziweze kuleta matokeo chanya kwenye Sekta ya Elimu, ndio maana programu tunayoizindua leo inaonesha kwa vitendo kuwa Serikali tunatambua kwamba lazima tuwekeze zaidi kwenye mazingira ya kujifunzia na kufundishia lakini pia kuwatambua walimu kuwa ndio watu tunaowategemea kufanya elimu yetu iweze kwenda mbele” Amesema Mhe. Dkt. Biteko.

Akimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada za makusudi ili masuala yanayowahusu walimu nchini yafanyiwe kazi ili kuwapunguzia changamoto zinawazowakabili kwa lengo la kutatua changamoto za watoto mashuleni.

Aidha, Dkt. Biteko amesema Serikali inaendelea kufanya maboresha ya bajeti ya Elimu kwani kwa mwaka 2021 jumla ya shilingi Trilioni 4.7 zilitolewa na kuongezeka hadi shilingi Trilioni 5.7 sawa na asilimia 20.4 mwaka 2023.

Kuhusu ufaulu amesema kutokana na kazi nzuri ya walimu kote nchini, wamewezesha kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi kwenda sekondari kutoka 907,802 mwaka 2021 hadi 1,092,984 mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.4 sambamba na kuwapandisha vyeo walimu 227,383 pamoja na kuwabadilishia vyeo walimu 20

Dkt. Biteko ametoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuangalia utaratibu mzuri wa kuwapa motisha walimu mfano kutenga walau siku moja ya kuwapa motisha walimu badala ya kusubiri Mei Mosi ya kila mwaka lengo likiwa ni  kupata matokeo bora kwa wanafunzi. 

Akitoa maelezo ya awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushirika wa Elimu Duniani (GPE) ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete alisema Mfuko wa GPE umeshachangia Dola za Marekani milioni 330 nchini Tanzania na kwamba GPE inaunga mkono juhudi za Serikali kuboresha Sekta ya Elimu ili kila mtoto awe na ujuzi na maarifa na sasa Taasisi hiyo imeidhinisha ufadhili wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya programu.

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa, programu iliyozinduliwa ya Kuboresha Kada ya Ualimu (GPE TSP) inagusa sehemu mbalimbali katika Kada ya Ualimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha utoshelevu wa walimu, kutoa walimu bora, uwepo wa miundombinu, vitendea kazi, kuendeleza makazi ya walimu na motisha kwa walimu ijapokuwa Serikali inatekeleza haya nao GPE inakuja kuongeza nguvu na  kasi ya utekelezaji wa programu za Serikali ikiwemo Sera ya Elimu.

Naye Charlotta Ozaki Macias Balozi wa Sweeden nchini Tanzania amesema Washirika wa Elimu Duniani (GPE) wataendeleza ushirikiano na Tanzania ili kuhakikisha Programu ya Kuboresha Kada ya Ualimu inafanikiwa na kusema kuwa awamu ya tatu ya ufadhili inawalenga zaidi walimu kwa ajili ya kuwawekea mazingira wezeshi na endelevu ili kutoa elimu bora kwani haki ya kupata elimu ni haki ya kila mtoto.

Kwa upande wake Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika Sekta ya Elimu kwani uwekezaji alioufanya umeleta tija kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji lakini pia ameahidi kuendelea kusimamia masuala ya elimu nchini pamoja na mitaala na Sera iliyobereshwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Fomu za kujiunga na Kidato cha kwanza 2024 December 16, 2024
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.