Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Utoro shuleni na ufaulu duni wachangia kuzinyima halmashauri fedha za elimu

Imewekwa tar.: July 28th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mwanza

Serikali imesema halmashauri nyingi zimeshindwa kupata fedha nyingi za ruzuku zitolewazo na wafadhili kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) kutokana na halmashauri hizo kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa vikiwemo vigezo vya utoro shuleni na uwezo wa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu kuweza kusoma, kuhesabu na kuandika kulingana na vigezo vya kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Tixon Nzunda wakati wa ziara yake katika halmashauri za jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kukagua umaliziaji wa maboma yaliyojengwa na na serikali katika halmashauri hizo.

Amesema kigezo cha kwanza ni ufaulu wa wanafunzi shuleni ambapo kigezo kinachopimwa ni kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza, pili na la tatu ni uwezo wao wa kujua kusoma kuhesabu na kuandika kwa kuzingatia viwango vya kimataifa ambavyo ni maneno 50 kwa dakika moja.

“Kama watoto wanaweza kusoma maneno 50 vizuri, na wakawa wengi kulingana na tathmini zilivyofanyika, halmashauri hiyo inapata fedha, wakibabaika babaika wako chini, wanaweza kupata kidogo ama sifuri, ” amesema.

Naibu Katibu Mkuu amesema kwa upande wa darasa la nne ufaulu unapaswa kuwa ni wa asilimia 100 ndiyo malengo ya nchi, darasa la saba kiwango cha ufaulu lazima kiwe juu ya asilimia 80 na endapo ufaulu utakuwa chini ya asilimia 80, halmashauri inaweza kupata fedha kidogo au kupata alama sifuri.

Kwa upande wa shule za sekondari, Naibu Katibu Mkuu amesema kigezo cha ufaulu ni kwa wanafunzi wote wa kidato cha pili kufaulu kwa asilimia 100, huku kwa kidato cha nne ufaulu unapaswa kuwa wa daraja la kwanza hadi la tatu uwe zaidi ya asilimia 50, na kwa upande wa kidato cha tano na cha sita ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu unapaswa kuwa wa asilimia 100.

“Jambo lingine ambalo mnapimwa nalo, na hili ni la wanasiasa, na wewe mama mwenye shule ni retension rate ya watoto ambapo inatakiwa watoto walioanza tangu elimu ya awali wafike hivyo hivyo hadi darasa la saba,” amesema na kuongeza:

“ Watoto walioanza form one (kidato cha kwanza) wafike hivyo hivyo form four na form six, Mhe Diwani, na mwenye shule, mwenyekiti wa kijiji na mwenyekiti wa kitongoji mkifeli kuwafanya watoto wenu wafike shuleni mnapata sifuri kwa sababu wenzenu hapa wanapata zaidi ya shilingi milioni 150” amesema

Bwana Nzunda ameeleza kuwa shule isipowabakisha watoto hao  shuleni, na kwa vile fedha hizo ni za wafadhili zinabaki kwao.

“Kwa hiyo mhe.Diwani, kupanga ni kuchagua na sisi tumechagua fedha zibaki hapa, na hiyo ni kazi ya siasa, kazi ya Mtendaji wa kata, kazi ya afisa tarafa, kazi ya Mkuu wa Wilaya, kazi ya jamii wenye shule kuhakikisha kuwa wanawashirikisha wazazi, na tunatumia nguvu kidogo ya kuhakikisha watoto wanabaki shuleni” amesema bwana Nzunda.

Naibu Katibu Mkuu ametaja kigezo kingine kinachopimwa ni upangaji wa walimu, kuna walimu wamejaa huko sekondari.

“Ni jukumu lenu kupitia baraza la madiwani kuamua kutenga fedha zitakazowezesha kuhamisha baadhi ya walimu hawa waliozidi shule za sekondari waende kule shule za vijijini kwenye mapengo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.