• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Unguja watamba kuchukua kombe UMISSETA

Imewekwa tar.: June 25th, 2021

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Kama kuna timu inayopaswa kutupiwa jicho la pili katika michuano inayoendelea ya UMISSETA basi ni timu ya mpira wa kikapu ya wavulana kutoka visiwani Unguja.

Tayari timu hiyo imekwishatembeza vipigo kwa timu mbili mashuhuri za Tanzania bara ikiwemo Kilimanjaro ambayo leo ilikubali kufungwa vikapu 38-21.

Timu hiyo ya Unguja inayonolewa na Mwalimu Nassoro Salum imekuwa ikitoa burudani safi kwa wakazi wa Mtwara na mikoa ya jirani wanaofurika katika viwanja vya Basketball vya Chuo cha Ualimu Mtwara kushuhudia umahiri wa wachezaji kutoka visiwa vya Unguja.

Katika mechi ya fungua dimba timu hiyo ya Unguja iliifunga Tanga kwa vikapu 48-30.

Mwalimu Salumu anakiri kuwa kinachowasaidia timu yake ni kuwa na wachezaji wazuri wanaopata fursa ya kucheza mara kwa mara katika timu za mitaani huko Zanzibar ukiachilia timu zao za shule.

Matokeo ya michezo mingine ya basketball iliyochezwa leo ni kati ya Geita dhidi ya Kigoma 25-28, Kigoma dhidi ya Dar es salaam 28-101 na Shinyanga dhidi ya Mbeya 60-40.

Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana Songwe walicheza dhidi ya Tabora ambapo  Songwe ilifungwa vikapu 15-36, na Ruvuma dhidi ya Iringa, Ruvuma ilishinda kwa vikapu 31-7.

Matokeo ya soka wavulana katika makundi tofauti yanaonyesha Kilimanjaro  iliifunga Pwani magoli 2-1, Ruvuma ilikubali kipigo cha magoli 0-3 kutoka kwa Tabora, Mbeya iliifunga Kagera goli 1-0 na Singida ilifungwa goli 1-0 na Arusha.

Mikoa ya Songwe na Shinyanga ilitoka sare ya kufungana goli 1-1, Morogoro iliichapa Simiyu magoli 2-1, Lindi na Dodoma zilitoka sare ya goli 1-1, Katavi ikaifunga Kigoma 1-0, Unguja ikaichapa Rukwa magoli 2-0, huku Mwanza na Njombe zikitoka suluhu, kadhalika kwa mchezo kati ya Tanga na Iringa nazo zilitoka sare ya bila kufungana.

Matokeo mengine ya soka wavulana ni mchezo kati ya Tabora dhidi ya Mtwara ambapo Mtwara ilihinda goli 1-0, Kilimanjaro ilikubali kipigo kutoka kwa timu ya mkoa wa Mwanza baada ya kukubali kichapo cha magoli 0-3, Kagera ikifungwa na Mara kwa magoli 1-2, sawa na mchezo kati ya Songwe dhidi ya Dodoma ambapo Songwe ilifungwa magoli 1-2.

Mchezo kati ya Manyara dhidi ya Iringa ulitoka kwa sare ya goli 1-12, Simiyu dhidi ya Geita 0-0, Katavi dhidi ya Singida 0-3, Rukwa dhidi ya Morogoro walitoka suluhu ya bila kufungana sawa na mchezo kati ya Lindi dhidi Mbeya ambapo walitoka suluhu ya bila kufungana.

Katika mchezo wa Netiboli matokeo Mwanza imeichapa Rukwa magoli 53-7, Geita imeifunga Simiyu magoli 41-19, Mbeya imeifunga Katavi magoli 24-14 na Tanga imeichapa Kigoma magoli 35-20.

Matokeo ya mpira wa mikono wasichana Geita dhidi ya Simiyu 24-17, Shinyanga  dhidi ya Morogoro 5-20, Dar es salaam dhidi ya Mbeya 11-15, Unguja dhidi ya Iringa 30-6, Tanga dhidi ya Ruvuma  26-6, na Rukwa dhidi ya Njombe 10-7.

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa mikono wavulana Songwe dhidi ya Tanga 10-19, Shinyanga dhidi ya Iringa 16-11, Kagera dhidi ya Rukwa 9-19, Geita dhidi ya Arusha 26-27, Mwanza dhidi ya Ruvuma 29-16, Manyara dhidi ya Pwani 16-24, na Morogoro dhidi ya Tabora 17-20.

Pia Dodoma iliifunga Kigoma 22-20, Mbeya ikaifunga Lindi 32-13, Singida dhidi ya Dar es salaam 16-32, Simiyu dhidi Unguja  12-48 na Kilimanjaro 11-13.

Matangazo

  • Orodha ya Majina ya Waliopata Ajira Kada za Afya na Elimu Juni 2023 June 05, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MANYARA, MARA ZANG'ARA UMITASHUMTA

    June 08, 2023
  • DKT.MPANGO AAGIZA UBORESHAJI MICHEZO MASHULENI

    June 08, 2023
  • HATUHITAJI MAMLUKI MICHEZO YA UMITASHUMTA-Dkt. Msonde

    June 08, 2023
  • MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA SHIRIKIANENI NA WANANCHI KUTATUA KERO ZAO

    June 06, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.