Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TRILONI 1.49 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO TAMISEMI

Imewekwa tar.: March 1st, 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais  Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya Rais- TAMISEMI imepokea jumla ya Shilingi trilioni 1.49 kwa ajili utekelezaji wa miradi  ya maendeleo katika Sekta ya Elimu, Afya na Barabara.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Machi 01, 2021 wakati akieleza  mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita kwenye kikao kazi cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara na waandishi wa habari.

Amesema katika Sekta ya elimu  kiasi cha shilingi  bilioni 662.32  zimetumika kujenga shule mpya 257 za sekondari na shule 9 za msingi,kujenga vyumba vya madarasa 18,219 kwa shule za msingi; Vituo Shikizi na Shule za Sekondari; ukamilishaji wa  ujenzi wa vyumba vya madarasa 4,525 kwa shule za msingi na sekondari, ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara 1,399 na  matundu ya vyoo 568 kwa shule za msingi na sekondari.

Waziri Bashungwa ameendelea kusema kuwa fedha hizo zimeweza ukamilishaji wa  mabweni 170 , nyumba za waalimu 42, kwa shule za msingi na sekondari, ujenzi wa  Maabara 11 kwa shule za sekondari, Mabwalo 6 kwa shule za sekondari, majengo ya utawala 4 kwa shule za sekondari na ukamilishaji wa Shule Kongwe nne (04) shule za msingi na sekondari.

Aidha, Amesema katika Sekta ya Afya serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni  234.41  kwa ajili ya ujenzi wa  Vituo vya Afya 288, Ujenzi wa Hospitali Mpya 28, Ujenzi wa majengo ya Wagonjwa Mahututi 26, Ujenzi majengo ya Dharura 80, ujenzi wa Kituo kimoja cha Matibabu ya Magonjwa ya Milipuko, ujenzi wa Nyumba 150 za watumishi katika maeneo ya pembezoni, ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati 615, Hospitali 68 za Halmashauri zilizoanza kujengwa Mwaka wa fedha 2018/19, ujenzi wa Hospitali 31 za Halmashaurii na Ununuzi wa Vifaa na Vifaa Tiba kwa Hospitali 31.

Vile vile, Waziri Bashungwa  amesema katika sekta barabara Shilingi bilioni 597 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi, matengenezo na ukarabati wa barabara za Wilaya zinazosimamiwa na TARURA, ambazo zimetumika katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 213.36, Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe zenye urefu wa kilomita 1,152.33, Matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 25,059.4, Ujenzi wa madaraja 201 ambapo ujenzi unaendelea,Ujenzi wa maboksi kalavati 70 na Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa kilomita 123.05.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.