Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TARURA YAANZA KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA - MALINYI

Imewekwa tar.: May 24th, 2024



#Takriban Km. 53 za barabara zapata madhara ya kukatika 


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa la kurekebisha haraka barabara zilizokatika wilayani Malinyi ili kurejesha huduma kwa wananchi.


Naibu Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu OR-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila amefika eneo lililoathiriwa na mvua na kuhimiza utekelezaji wa haraka ndani ya muda uliopangwa.


“Mhe. Waziri Mchengerwa alitembelea barabara na madaraja yaliyokatika kutokana na athari za mvua na kujionea barabara hii ya Lugala-Misegese ikiwa imekatika na kusababisha magari kutopita na  akaelekeza mara moja barabara hii irekebishwe na mimi kama Naibu Katibu Mkuu ninayeshughulikia miundombinu nimefika  nione hali ipoje na tunarekebishaje haraka kwani Waziri alitoa pia maelekezo kwamba fedha zitolewe, fedha zipo na mkandarasi apatikane kurekebisha eneo hili".


Aidha, amesema moja ya barabara iliyopata changamoto ni barabara inayoenda kwenye hospitali ya wilaya kutokana na dharura hiyo imebidi wamchukue mkandarasi aliyepo jirani afike na aanze kufanya kazi na tayari mkandarasi huyo ameanza kupeleka vifaa kama alivyoagiza  Mhe. Waziri kwa kutoa siku nne mkandarasi apatikane na aanze kazi kuhakikisha panapitika.


“Tunategemea ndani ya hizo siku nne alizopewa angalau wananchi waweze kupita kwa magari wakati marekebisho makubwa yanaendelea. Na mimi nimeliona hilo naenda kulisimamia haraka, wakituletea tu maombi ya fedha, fedha hizo tutazileta mkandarasi yupo hapa tayari kuanza kazi", amesema.


Vile vile ameiagiza TARURA kusimamia kazi hiyo usiku na mchana ili ikamilike haraka na mkandarasi aweke wafanyakazi na vifaa vya kutosha.


Naye, Katibu Tawala Wilaya ya Malinyi, Bi. Saida Mhanga amesema barabara ya Malinyi - Igawa wanaitumia kuelekea ofisini na nyenzo kuu inayotumika hivi sasa ili waweze kufika kazini ni pikipiki. Hivyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea milioni 800 kwa ajili ya kurekebisha mawasiliano wilayani hapo.


Amesema kwa asilimia 95 ya chanzo kikubwa cha mapato wilaya ya Malinyi ni kilimo ikiwemo ufuta, mahindi, choroko na mengineyo hivyo kurejesha barabara hayo itawasaidia wakulima katika msimu huu wa mavuno.


Mhandisi Charles Mang’era Meneja TARURA Wilaya ya Malinyi amesema wilaya hiyo ni kati ya wilaya ambazo zimepata madhara makubwa kutokana na mvua za masika zilizoanza Novemba mwaka jana mpaka katikati ya Mei mwaka huu hivyo miongoni mwa madhara ambayo yamejitokeza katika wilaya yao ni miundombinu kukatika.


“Takriban Km. 53 za barabara zimepata madhara ya kukatika, miongoni mwa ambazo zimeathirika zaidi ni hii ya Malinyi – Igawa na Lugala –Misegese, Serikali imekuwa sikivu wametupatia Shilingi Mil. 800 fedha za dharura kuhakikisha barabara zote mbili zinafunguka na wananchi wanapata huduma”.


Wakati huo huo Mkurugenzi wa ufundi kutoka kampuni ya Bavaco Mellezier Limited Mhandisi Nkolate Ntije amesema tayari wameshapeleka vifaa muhimu kwaajili ya kuanza utekelezaji wa kurejesha mawasiliano ya barabara hizo na kuongeza kwamba wanaishukuru Serikali kwa kuwaamini na kuahidi kukamilisha kwa muda waliopewa.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.