Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TAMISEMI NA MPANGO WA SHULE SALAMA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI KWA WANAFUNZI

Imewekwa tar.: August 5th, 2024

Na OR – TAMISEMI, Iringa

Ili kukabiliana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi, utoro na ukosefu wa chakula mashuleni Ofisi ya Rais TAMISEMI imekuja na Mpango wa Shule Salama, mpango utakaosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuwawezesha kufikia ndoto zao za kielimu

Akizungumza katika mafunzo ya wakufunzi wa Mpango wa shule salama yaliyofanyika mkoani Iringa, Maratibu wa mpango huo kitaifa, Bi. Hilda Mgomapayo alisema utafiti umebaini kuwa zipo changamoto zinazochangia wanafunzi wa shule za sekondari washindwe kumaliza mzunguko wao wa elimu na kuathiri ndoto zao,ambapo miongoni mwa changamoto hizo zinasababishwa na wazazi,jamii na walimu

‘’mpango huu unalenga kubadilisha mitazamo,tabia na mwelekeo wa jamii kwa ujumla dhidi ya watoto ili tuweze kuwalinda na kuwaepusha na vitendo vya ukatili ili tuwawezeshe kukamilisha mzunguko wa elimu”alisema Mgomapayo

Alisema lengo la serikali ni kupunguza vikwazo hivyo kwa wanafunzi na kufanya shule kuwa eneo salama kwa mtoto kufikia ndoto zake kupita mpango wa shule salama nchini ambao ni mpya na unaratibiwa na Wizara ya nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI chini ya Mradi wa kuboresha shule za sekondari SEQUIP.

“baada ya mafunzo haya ya wawezeshaji wa kitaifa tunategemea wataenda kuwawezesha watekelezaji wa mpango huu katika ngazi za Mikoa, Wilaya hadi Kata ambao watakuwa ni Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata ambako ndiko jamii ilipo, watafanya ulaghibishi na uchechemzi na mafunzo kwa jamii” alisema Bi. Mgomapayo.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Reginaldo Msendekwa na Saida Mgeni walisema Mpango wa shule salama umekuja wakati muafaka ambapo wanafunzi wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokea majumbani hadi mashuleni.

“kimsingi shule salama ni jumla ya mahitaji yote anayoweza kuyapata mwanafunzi ikiwemo chakula, malazi, vitendea kazi pamoja na uwepo wa mazingira mazuri ya kujifunzia,haya yote yanaweza kufanya mtoto kuwa salama na kufanikiwa kufikia ndoto zake kwani anapoyakosa analazimika kuyatafuta nje ya utaratibu na ndiyo maana wengi wanafanyiwa ukatili” walisema.

Pamoja na mambo mengine ya kuboresha elimu Mpango huo pia utasaidia kuimarisha utoaji wa chakula mashuleni na kuzingatia miundo mbinu ya mahitaji maalum. 


Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.