Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

SWEDEN KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA KWENYE MIRADI YA GPE NA LIPA KULINGANA NA MATOKEO (EP4R)

Imewekwa tar.: November 20th, 2024

 Na Fred. Kibano, Arusha

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mheshimiwa Charlota Marcias alisema Serikali ya Sweden itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo katika kuendeleza elimu kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali zinazoonekana kwenye Sekta ya Elimu nchini.

Mhe. Charlota Marcias aliyasema hayo Jijini Arusha leo Tarehe 20 Novemba, 2024 katika Shule ya Msingi Muriet Darajani iliyopo Jijini Arusha mkoani Arusha na kusisitiza kuwa urithi mkubwa wa Watoto ni elimu na ndiyo maana Sweden inaendelea kuunga mkono jitihada za utoaji elimu nchini kwenye miradi ya elimu hususani miradi ya GPE na Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).

Aidha, Mhe. Charlota alisema kwa sasa kipaumbele kikubwa ni kuboresha eneo la ufundishaji na ujifunzaji wa walimu na wanafunzi kwenye maeneo ya utoaji wa vitabu, Mafunzo ya Walimu Kazini (MEWAKA) na ujenzi wa miundombinu ambayo itawafanya walimu waweze kuboresha utoaji wao wa elimu kwa wanafunzi hapa nchini.

Akiongea kwa niaba ya Serikali Dkt.  Mahera Wilson Charles ambaye ni Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameiwezesha Sekta ya Elimu kusonga mbele kwa kujenga miundombinu mipya na kutoa vitabu ambavyo vimeboresha uwiano kati ya wanafunzi na vitabu kote nchini.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muriet Darajani Dominick Gado amesema shule yake ilipokea kiasi cha Shilingi 55,824,000 zilizojenga madarasa mawili ya mfano na samani zake, kuweka bembea, ununuzi wa vifaa vya michezo kwa ajili ya Watoto wa awali, matundu sita ya vyoo na tenki la maji safi lakini pia kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) shule yake ilipokea Shilingi 108,800,000 ambazo zilijenga vyumba vitano vya madarasa ambavyo vimepunguza msongamano shuleni hapo.

Ziara hiyo ya kikazi ya siku nne kati ya Serikali na Ubalozi wa Sweden inalenga kuangalia ufanisi wa Mradi wa GPE LANES II na Programu ya EP4R kwenye mikoa ya Arusha na Mara. Pia upo Mradi mpya ulioanza wa Kuboresha Kada ya Ualimu (GPE TSP) wenye lengo la kuboresha Kada ya Ualimu nchini.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.