Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Siku 7 za kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za Uongozi

Imewekwa tar.: October 28th, 2019

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo, kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali wa Mitaa 2019 ametangaza rasmi siku saba za kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea kwa nafasi mbalimbali katika ngazi za Vijiji, Mitaa, Vitongoji na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa kwa ajili ya uchaguzi serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu litaanza tarehe 29, Oktoba na litahitimishwa tarehe 4 Novemba, 2019, zoezi ambalo litakuwa la siku tisa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Jijini Dodoma, Waziri Jafo amesema zoezi hilo linahusisha wananchi  wenye sifa na ambao wamepitishwa katika vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu na waliokamilisha taratibu zote kwenye vyama vyao.

Mhe. Jafo pia amewataka  wananchi wote  wenye nia ya kuongoza katika serikali za Mitaa kutumia siku zilizowekwa kikamilifu kwa kwenda kuchukua fomu za kugombea kupitia vyama vyao.

“Zoezi hili litaanza rasmi kesho tarehe 29/10 na litahitimishwa siku ya tarehe 4/11, 2019, na watakao takiwa kugombea ni wale wanaotoka katika vyama vyenye usajili wa kudumu na waliopitishwa na vyama vyao” amesema Waziri Jafo.

Aidha amesema maandalizi yote kwa ajili ya zoezi hilo yamekamilika, na kuwataka watu wote wazingatie kanuni na taratibu wakati wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo na kuwataka wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi kusimamia kikamilifu zoezi hilo.


Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ndio wasimamizi wa ulinzi na usalama katika maeneo yao  kuhakikisha wanaimarisha hali ya ulinzi na usalama wakati wote wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi.

Amebainisha kuwa ameshatoa barua ya ufafanuzi  kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuhusu namna ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu utakavyoendeshwa, na amevitaka vyama vyote vizingatie demokrasia wakati wote wa zoezi hilo.

Mnamo Oktoba 22, 2019 Mhe. Jafo alitoa maelekezo kuwa viongozi wa vijiji, vitongoji, Mitaa, na wajumbe wote kuwa uongozi wao ulikoma tarehe hiyo na kwamba shughuli zote zinazohusu ngazi hizo zitafanywa na watendaji wa vijiji,Mitaa, Kata na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Amesema “kuanzia tarehe hiyo wenyeviti wa Mitaa,vijiji, vitongoji na wajumbe, hawataruhusiwa kutekeleza majukumu  yeyote kwenye maeneo yao, badala yake Kama kutakuwa na Jambo wanapaswa kushirikiana na kuamuliwa na mtendaji wa Kijiji, Kata na Mkurugenzi wa Halmashauri” amesema,

Jafo alimalizia kuwakumbusha wagombea wote watakajiotokeza kwenda kuchukua fomu  kuwa kufanya kampeni za uchaguzi kabla ya muda wake hairuhusiwi hivyo zoezi la kwenda kuchukua fomu linaweza kuambatana na mbwembwe lakini  zisiwe na muelekeo wa Kampeni.

Mwisho.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.