• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali yatumia takribani shilingi Trilioni 3.5 ujenzi wa miundombinu Serikali za Mitaa.

Imewekwa tar.: August 5th, 2020

KATIKA kipindi cha miaka mitano, Serikali imetumia takribani Sh trilioni 3.463 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo wakati wa kuelezea mafanikio katika sekta ya miundombinu ikiwa ni siku ya tatu ya maadhimisho ya Siku ya TAMISEMI.

Amesema fedha hizo zikiwamo Sh trilioni 1.03 zilizoelekezwa  kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na Sh trililioni 1.98 ambazo ni fedha maalumu zilizotumika kujenga mtandao wa barabara za lami katika miji ya kimkakati, Manishaa na Halmashuri za Miji na Jiji la Dar es Salaam.

Amesema  hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa mtandano wa barara za lami kwa mamlaka ya serikali za mitaa kwa urefu wa kilimita 699.5 ambayo ni asilimia asilimia 52 kutoka kilomita 1,325.49 mwaka 2015 hadi kufikia kilimita 2,024.99 mwaka 2020.

Amesema kwa upande wa barabara za changarawe kwa Mamalaka za Serikali za mitaa kulikuwa na barabar zenye urefu wa kilomita 22,089 na baada ya maboresho zimefikia urefu wa kilomita 24,193 ikiwa na ongezeko kwa asilimia 11 huku serikali ikiimarisha barabara za vumbi(udongo) na kufikia urefu wa kilomita 82,428 wakati madaraja makubwa yaliyojengwa ni 99.

“ Mtandao wa barabara zenye hali nzuri na wastani  umeongezeka kutoka kilomita 61,798.45 hadi kufikia kilomita 63,164.74 sawa na ongezeko la barabara zenye hali nzuri na wastani urefu wa kilomita 1,366.29, hii inafanya barabara zenye hali nzuri kutoka asilimilia 56 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 58 mwaka huu,”

“Hii inaonesha utashi wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wa kuhakikisha wananchi wanatengenezewa mtandao wa barabara na hii imesahidia hata wakulima kuweza kusafarisha mazao yao, siku za nyuma watu walikuwa wanateseka sana, tunamshukuru Rais kwa kuwezesha hili.” Amesisitiza  Mhe. Jafo

Akifafanua zaidi anasema  mbali na barabara, lakini pia Serikali imewezesha ujenzi wa stendi za kisasa 24, stendi za malori, masoko ya kisasa  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa , madapo ya kisasa katika baadhi ya Miji.

Kuhusu  mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es Salaam (DART), Mhe. Jafo  amesema ikiwa kazi za awamu ya pili ya mradi huo ikishika kasi, awamu ya kwanza imekuwa na mafanikio ya kuongeza abiria kutoka watu 75,000 kwa siku hadi kufikia abiria zaidi ya 200,000 kwa siku.

“ Bado tunaendelea na maandalizi ya kumtafuta mtoa huduma wa kudumu atakayekuwa na uwezo kutoa huduma ya mabasi 305 ikilinganishwa na mtoa huduma wa sasa ambaye ana uwezo wa kutoa huduma ya mabasi 140.”amesema Mhe. Jafo

Naye Meneja wa Mfuko wa Barabara,  Eliud Nyauhenga amesema  magari kuzidisha mzigo ni moja ya changamoto inayorudisha nyuma juhudi za serikali katika maendeleo ya sekta ya barabara.

“ Uzidishaji mizigo kwenye magari kinyume na matakwa ya sheria imekuwa ikichangia sana uharibidu wa barabara, mfano kwa sasa huko vijijini magari yanayokwenda kubeba mazao wamekuwa wakizidisha uzito jambo ambalo linaharibu miundombinu.” Anafafanua Nyauhenga


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.