• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Serikali Yakabidhi Hosteli kwa Chuo Cha Mipango Dodoma

Imewekwa tar.: September 18th, 2019

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amekabidhi majengo na eneo lililokuwa linamilikiwa na halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.

Akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano ya majengo na eneo hilo yaliyopo katikati ya Jiji la Dodoma eneo la barabara ya kuelekea Iringa, Mhandisi Nyamhanga amesema awali majengo hayo yalikuwa yakimilikiwa na lililokuwa Shirika la Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) na baada ya kuvunjwa kwake yalikabidhiwa kwa halmashauri ya Jiji la Dodoma na Chuo cha Mipango walikuwa wapangaji katika majengo hayo.

“Chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Maendeleo Vijijini kilikuwa kinapanga hapa na kilikuwa kinalipa gharama kubwa naambiwa zaidi ya shilingi milioni250 kwa mwaka kwa ajili ya wanafunzi kusoma, lakini sasa Serikali imeamua kwamba hosteli hii ikabidhiwe kwa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo Jijini Dodoma”

Makabidhiano hayo yamefanyika leo hii kwa kubadilishana hati kati ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kwa niaba ya Serikali na Mkuu wa chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya.

Mhandisi Nyamhanga amemtaka Mkuu wa chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Maendeleo Vijijini kukarabati majengo hayo lakini pia kuondoa majengo ya muda yaliyokuwa yakitumiwa kama madarasa na kujenga majengo mapya ya kudumu kwa kuwa sasa hawapangi tena na wao ndio wamiliki.

Amewataka wanafunzi wote wa chuo hicho kusoma kwa bidii na kuinua kiwango cha ufaulu lakini pia kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amekuwa mstari mbele na kufanya jitihada kubwa za kuboresha elimu kuanzia shule za awali, msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya ameishukuru Serikali kwa maamuzi mazuri ya kuwakabidhi majengo hayo na eneo ambalo litasaidia kuboresha miundombinu na mazingira rafiki ya kujifunzia kwani gharama za upangaji katika majengo hayo zilkuwa kubwa ambazo ni zaidi ya milioni 252 kwa mwaka.

Katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma aliwakilishwa na Elihuruma Mufuruki Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Jiji la Dodoma.

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya bado kina uhitaji wa miundombinu ya majengo ya madarasa na hosteli kutokana na kudahili wanafunzi wengi kutoka mikoa karibu yote hapa nchini.

Anaandika Fred Kibano


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.