• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Serikali yagawa Pikipiki 2894 kwa Waratibu Elimu Kata nchini

Imewekwa tar.: July 4th, 2018

Serikali imezindua zoezi la usambazaji wa pikipiki 2,894 kwa Waratibu Elimu kata nchini kwa kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha kuwa pikipiki hizo zinawafikia walengwa hao.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa funguo za pikipiki hizo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo, amewataka Maafisa wa Elimu kuhakikisha kuwa pikipiki hizo aina ya Honda zitumiwe na Waratibu Elimu kata.

Alisema kuwa serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli imelipa uzito suala la utoaji wa elimu bora nchini ndiyo maana serikali imeamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu bila malipo.

“Ni matumaini yangu baada ya serikali kukubali kutoa pikipiki hizi suala la usimamizi wa elimu katika kata zenu litaenda kufanyika vizuri bila visingizio vyovyote,” alisema.

Mhe.Jafo alisisitiza kuwa  serikali inaenda kuwapatia waratibu wa elimu kata pikipiki hizo na kamwe pikipiki hizo zisitumiwe kwa ajili ya shughuli nyingine zozote mbali na ufuatiliaji na usimamizi wa shule katika kata husika.

“Napenda kulisisitiza jambo hili, pikipiki hizi siyo za kuendea kwenye viti virefu, na pia zisitumike kufanyia shughuli ya bodaboda,” alisema Mhe.Jafo.

Aidha aliwataka Maafisa Elimu Wilaya kuhakikisha kuwa pikipiki hizo aina ya Honda ndiyo zitakazogawiwa kwa waratibu elimu kata na si vinginevyo.

“Sitaki kusikia kuwa waratibu wa elimu kata wamegawiwa pikipiki za aina nyingine badala ya aina hii ya Honda tunazozigawa leo,” alisema.

Alisema serikali inalenga kupandisha ubora wa elimu katika ngazi ya kata, hivyo amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha kuwa pikipiki hizo zinapatiwa huduma ya mafuta bure katika kipindi cha miezi sita.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa pikipiki hizo zilinunuliwa na Wizara yake kupitia programu ya Lanes ambapo serikali imehakikisha kuwa pikipiki hizo ina vifaa vyote vya usalama barabarani.

Alisema kuwa ni matarajio yake kuwa pikipiki hizo zitawawezesha waratibu elimu kata kuboresha ubora wa elimu katika kata kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara katika shule zao.

Alisema kuwa hatarajii kuona wanafunzi wengi wanaendelea kupata daraja la sifuri, na kamwe shule zisiwe vituo vya kulea watoto badala yake kata ziimarishe usimamizi wa elimu.

Mapema Mwakilishi wa wadau wa Maendeleo Bibi Susan Steven alisema kuwa wao kama wadau wa maendeleo  wamefurahishwa na hatua ya serikali kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya elimu Tanzania.

Anaandika  Mathew Kwembe  OR TAMISEMI

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BARABARA YA MVUMI KUWEKWA LAMI KM 3

    May 26, 2022
  • PROF. SHEMDOE AZINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI 8 KWA KUTOKUTENGE FEDHA ZA LISHE

    May 25, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA ASIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA JIJI, MAAFISA WATANO ARUSHA

    May 24, 2022
  • WAKUU WA MIKOA SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE HALMASHAURI

    May 24, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.