Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali Yaagiza Wakurugenzi 31 Kutenga fedha za Lishe

Imewekwa tar.: March 19th, 2019

Serikali imetoa siku 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri 31 ambao hawakutoa fedha kwa ajili ya usimamizi wa masuala ya lishe katika Mamlaka za Serikali za Mitaa watoe taarifa na kuiwasilisha kwa Wakuu wao wa Mikoa ambao pia watatakiwa kuiwasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI ndani ya siku 21.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo wakati akifungua mkutano wa pili wa tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe nchini uliosainiwa baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wakuu wa mikoa ya Tanzania Bara Desemba, 2017 ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2018.

“nazipa siku 14 halmashauri 31 ambazo zimeshindwa kutoa fedha za usimamizi wa masuala ya lishe kutoa maelezo kwanini hawakufanya hivyo, pia taarifa hiyo iwasilishwe kwangu na Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa ndani ya siku 21, hii inasababisha shughuli za lishe zisiende vizuri nchini“

Mhe. Jafo amesema utekelezaji wa mikataba ya lishe uwe ni suala endelevu na sio tu kama sehemu ya utekelezaji wa shughuli za kila siku kwani nchi haitafikia malengo yake ya kuwa Taifa shindani.

Aidha, ameagiza Wakurugenzi kuwafuatilia Wakuu wa Idara ambao wanawatuma Maafisa kuwawakilisha katika vikao vikubwa wakati hawana maamuzi yoyote ili kuboresha utendaji kwa kupitisha maamuz kwa wakati.

Pia amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kuwaandikia Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza agizo lake la vyakula vyote vinavyopelekwa na wazabuni  katika shule na Wazabuni viwe na virutubisho ili kuboresha lishe za wanafunzi.

Amependekeza mwezi wa Agosti kuwa na tarehe ya kuadhimisha siku ya Lishe nchini ili Taifa liweze kujadili masuala ya lishe na kujenga jamii bora ya Watanzania.

Kwa upande wake Mhe Josephat S. Kandege Naibu Waziri (Afya OR - TAMISEMI) amesema kuwa upimaji ujao utakuwa mzuri kwani wote wanafanya vizuri lakini pia kuanza kutegemea bajeti yetu sisi wenyewe.

Awali akitoa maelezo kabla ya ufunguzi wa mkutano kazi huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema kuwa chimbuko la lishe ni lishe duni ambayo imekuwa ikiwakabili watoto wpatao asilimia 34 sawa na watoto milioni 30 nchini, watoto walio chini ya miaka mitano kuwa na upungufu wa damu, ukondefu wa watoto na upungufu wa damu kwa akina wanaotarajiwa kujifungua na waliojifungua.

Nyamhanga amesema kuhusu changamoto kwa baadhi ya halmashauri kutokuwa na Maafisa Lishe, tayari ameiagiza mikoa na halmashauri hizo kuweka katika mpango wa bajeti ili Maafisa hao waweze kuajiriwa kukabiliana na upungufu uliopo. Aidha, amesema utekelezaji wa masuala ya lishe umefikia asilimia mia moja katika mikoa ijapokuwa mafanikio yanatofautiana kati ya mkoa mmoja hadi mwingine.

Naye Bw. Kilumba Wakulichombe ambaye ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, amesema kuwa zipo hospitali maalum ambazo zinahudumia watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambazo ni Taasisi ya Mifupa Dar es Salaam (MOI), hospitali ya Rufaa Bugando (Mwanza), hospitali ya KCMC (Kilimanjaro), hospitali ya LCM (Arusha), hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya na hospitali ya HYDOM mkoani Manyara.

                            Anaandika Fred Kibano


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.